Ama kweli vimbwega haviishi katika muziki wa Kibongo.
Ni ajabu kidogo
baraza la sanaa la Taifa BASATA, lenye dhamana ya kusimamia sanaa ya taifa kumtambua Cyrill Francisco aka Kamikaze mzaliwa
wa Kiomboi, Singida kama 'mkenya'.
Kitendo hicho kimesababisha katibu mtendaji wa BASATA Ghonche
Materego kuwaandikia barua kali wamiliki wa ukumbi wa New Maisha Club kwa kumleta msanii kutoka Kenya (Cyrill ambaye ni
mtanzania hata hivyo) bila kibali na hivyo kuuzuia uzinduzi wa documentary yake
FROM DAY ONE kesho (May 20).
“Katika vyombo vya habari umetangaza kumleta msanii Cyrill
kutoka Kenya kufanya onesho tarehe 20/05/2012 bila kibali cha Serikali.
Huu ni ukiukwaji wa makusudi wa taratibu zilizowekwa na
serikali na hivyo unaamriwa kusimamisha zoezi hilo na ueleze kwa maandishi
kwanini usichukuliwe hatua za kishiria kwa ukiukwaji huo.
Maelezo yawe yamefika BASATA siyo zaidi ya tarehe
25/05/2012.” Inasema barua hiyo.
Gonche Materego (wa kwanza) |
Akionesha mshangao wa
issue nzima Cyrill leo amesema “eti wanasema
NIMETENGENEZA skendo...huu ndio uthibitisho namba 1,namba 2 ni mazungumzo ya
simu baina yangu na bosi wa BASATA leo mkuu Bwana LUHALA yaliyorekodiwa muda
wowote ntayaweka hewani wananchi wenyewe mjaji tasnia yetu inapelekwa wapi. Eti
wanasema mimi sio mbongo well wamepotea njia vibaya sana...#ILA WAJUE TU SHOW
IPO KAMA KAWAIDA kesho pale Maisha Club Oysterbay..from WAKACHA ENT.
Jana msanii huyo aliandika "Inasikitisha kuona kwamba Tanzania bado kuna fitina za
kurudishana nyuma kimaendeleo..sasa leo hii wanasema mimi sio mtanzania eti ni
mkenya wakati basata jina langu lipo..sasa kama ni tecnic yao kunifelisha
kwenye hii show wamepotea njia sababu,tarehe ni moja tu 20th may jumapili hii
tukutane maisha club..ha ha ha ha. #WAMEOGOPA!
Je! suala la BASATA
kumchukulia Cyrill kama msanii wa Kenya limetokana na uelewa mdogo wa
BASATA juu ya wasanii wake ama ni Fitina ya mtu anayetaka kukwamisha
uzinduzi wa Documentary yake?
0 MAONI YAKO:
Post a Comment