Rajabu mzigoni: Bwana Rajabu akimchuna mbwa kama alivyokutwa na kamera yetu.…
Rajabu mzigoni: Bwana Rajabu akimchuna mbwa kama alivyokutwa na kamera yetu.
Safari: Rajabu akimweka kwenye kiroba mbwa huyo tayari kwa safari.
Chini ya ulinzi: Rajabu akiwa kafungwa mikono baada ya kula kichapo.
UKISTAJABU ya Musa utaona ya firauni, hali hiyo iliwatokea wakazi wa Ubungo Kibangu pale mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Rajabu aliponaswa na wananchi akimchuna mbwa.
Baada ya Rajabu kufumwa akifanya kitendo hicho Jumamosi ya wiki iliyopita, alipewa kibano na wananchi wenye hasira kali akakiri kwamba mbwa huyo alikuwa akimuandaa ili akamuuzee kama mishikaki na supu kwa wateja wake.
Shuhuda wetu aliiambia blog hii kuwa baada ya wananchi kumtilia shaka anapopata nyama ya kuuza kutokana na hali yake ya kiuchumi kuwa duni, waliunda kikosi kazi cha kumchunguza ndipo arobaini yake ikatimia.
Mtoa habari huyo alisema baada ya wananchi kuchukizwa na kitendo hicho waliamua kumfikisha kijana huyo Kituo cha Polisi cha Kibangu.
“Kijana huyo alipohojiwa na polisi alikiri kufanya biashara hiyo kwa muda mrefu,” kilisema chanzo chetu.akiendelea kulipoti mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alisema kuwa taarifa juu ya tukio hilo hajazipata na akaahidi kuzifuatilia na kusisitiza kuwa kama ni kweli kijana huyo alifanya kitendo hicho atachukuliwa hatua za kisheria.
kwa hisani ya Grobalpubrishers
0 MAONI YAKO:
Post a Comment