
Vyama
vitatu vya wanasheria Afrika vimetoa tamko la pamoja kulaani kukamatwa
kwa Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS), Tundu Lissu
alipokuwa akielekea Kigali, Rwanda kwenye mkutano wa wanasheria wa
Afrika Mashariki.
Tamko
hilo limetolewa kwa pamoja na Chama cha wanasheria cha Afrika Mashariki
(EALS), Chama cha Wanasheria cha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC-LA) na Muungano wa Wanasheria Afrika (PALU).
Tamko
hilo lililosainiwa na Rais wa PALU, Elijah Banda, Rais wa Sadc LA, James
Banda na Rais wa EALS, Richard Mugisha limeeleza kwamba Lissu
alikamatwa kabla ya kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma dhidi yake ,
jambo ambalo ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
sheria nyingine za kimataifa.
Muungano
wa vyama hivyo umebainisha wazi kwamba mfululizo wa matukio hayo ni
mwanzo wa kuzorota kwa uhusiano kati ya TLS na serikali ya Tanzania.
"Kwa
kuwa suala hili liko mahakamani, hatutasema mengi kwa sasa, isipokuwa
tunazikumbusha pande zote kutambua uwepo wa sheria hasa zile
zinazotambua haki za binadamu. Tutaweka utaratibu wa kufuatilia
mashitaka dhidi ya Lissu," inasomeka sehemu ya tamko hilo.
Chanzo: Mwananchi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment