Ni producer toka mjini Morogoro katika studio za Mahewa Records zilizopo sabasaba. Ni mmoja katika maproducer wanaoaminika kutokana n ubora wa kazi zao.
Alianzisha studio ya Mahewa mwaka 2008. Willei Matajili anasema kazi ya kutayarisha nyimbo ni ngumu tofauti na wengi wanvyochukulia. Hasa unapofanya kazi na msanii mkubwa mara nyingi anataka ufanye kile anchotaka yeye japo ni bor lakini wanakuweka nje ya malengo yako.
Willei anasema kazi inakuwa ngumu zaidi unapofanya kazi na msanii mchanga, unatakiwa kutumia muda mwingi kumuelekeza ili kufanya kazi iliyo bora zaidi.
Willei Mtajili wa Mahewaaa akizungumza nami
Nyimbo ambazo zimefanya vizuri sana kutoka katika studio za Mahewa chini ya utayarishaji wake ni Sinyorita na Tutoke (Criss wamarya) ni wimbo ulofanya vizuri sana ktk vituo vya radio Tanzania na baadhi ya nchi za Africa Mashariki. nyingine Willei anajivunia ni Maskini afulii (Afande Sele na 20%)
Karbu Morogoro wa Moro All Star, Simuoni ( Koba MC),Kila nabii na nivumilie (Nassa) na wimbo unaotamba sasa na kufanya vizuri zaidi wa Kinyulinyuli (Sameer)
Mahewa Records zipo sabasaba manispaa ya Morogoro
Big up producer nakukubali sana
ReplyDeletemawasiliano yake nayapata vip?