ZITTO KABWE

Mbunge wa Kigoma kaskazini - CHADEMA Zitto Kabwe Zuberi ameamua kufunguka kuhusiana na RBT na madai ya serikali
Akifunguka kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto amesema
Zitto Kabwe
Serikali
inasema kampuni za simu zinalipa kodi nyingi. Kodi gani? VAT! Nani
kasema VAT inalipwa na kampuni? Hii Ni kodi ya walaji kama ilivyo ushuru
wa bidhaa (excise duty). Serikali inasema kampuni za simu hazilipi kodi
ya mapato Kwa kuwa zimewekeza sana, tshs 2.5 trilion! Nani kakagua huo
uwekezaji? Eti Kwa miaka 5 kodi ya makampuni iliyolipwa Ni tshs 64bn,
wastani wa tshs 12bn Kwa mwaka. Rwanda yenye idadi ya watu sawa na
wateja wa Vodacom peke yake mwaka 2010 walikusanya corporate tax $14m,
Tanzania ilikusanya $1.4m tu. Serikali iache blah blah, ikusanye kodi.
TCRA ipewe Nguvu ya kukagua uwekezaji wa makampuni kama ilivyo TMAA
kwenye madini. Inatosha sasa
0 MAONI YAKO:
Post a Comment