Wema Sepetu
Muigizaji
na Miss Tanzania wa zamani Wema Isac Sepetu amesema licha ya kumsainisha
Kajala Masanja kwenye kampuni yake, hategemei kumfanyisha kazi kurudisha
shilingi milioni 13 alizomtolea kwenye hukumu yake.
Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds fm leo, Wema amesema Kajala atakuwa akifanya
kazi zake lakini atakuwa akimlipa kama kawaida. Kwa kuanza Kajala
ataigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu iitwayo Princess Sasha.
“Tutaenda kuishoot nje ya Dar, ninataka kuishoot mandhari fulani hivi
kama ya kijijini. Ni mtoto wa mfalme, Kajala ndo atakuwa Princess
Sasha, she is going to be the main character, “ alisema Wema.
Kajala Masanja
Kwa upande wake Kajala amesema aliamua kujichora tattoo ya jina la Wema kwasababu anamchukulia kama shujaa wa maisha yake.
Sehemu ya mwili wa Kajala aliyochora Tatoo yenye jina la Wema
“Mi naweza kusema nimeichora kuonesha nimeappreciate vipi kitu
alichonifanyia , watu wengine wanaichukulia vibaya, wataongea vibaya,
lakini mimi najua moyoni mwangu. Sababu nimeona siwezi kumlipa hiyo hela
sasa hivi.
Ntamkumbuka siku zote hata chochote kikitokea atabakia kuwa
mtu… yaani she is my hero.”
Jumaamosi ijayo watakuwa club Embassador wakiwa na DJ Fetty na DJ Mully B tka Clouds fm. Watoa nafasi ya kupiga nao picha.
Chnzo: mpekuzi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment