Dayna Nyange
Siku kadhaa baada ya ktokea mlipuko wa bomu mjini Arusha na kusababisha kifo na majeruhi, msanii wa muziki wa bongo freva Dayna Nyange, amesema yake. Katika kauli yake Dayna amesema serikali inatakiwa kuchukua htua za haraka juu ya wahusika wa tukio lile pindi wakibainika.
''Kwakweli ni tukio la ajabu na lakusikitisha hasa kwa nchi yetu tunayoishi kijamaa, watanzania tumezoea kuishi kindugu, lakini sasa haya matukio yamezidi kwakweli. Amani tulio nayo ni ndogo lakini tutakuja kuikumbuka kwani tuangalie nci za wezetu, wanishi kama wahamiaji ndani ya nchi zao kutokana na tukio hili la kusikitisha, tunatakiwa watanzania wote bila kujali itikadi za dini wala siasa, kukemea mambo haya na ikibidi kuhamasisha serikalai wachukue maamuzi magumu ili kukomesha haya mambo"Amesema Dayna Nyange
TADB YAJITAMBULISHA KWA WAZIRI WA MIFUGO
-
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa( Mb.)
amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TABD) na...
1 hour ago






0 MAONI YAKO:
Post a Comment