Afande Sele akiwa na Madee siu ya msiba wa Ngwea
Msanii wa uziki wa Hip Hop toka mkoani Morogoro ambaye ndiye mfalme wa Rhymes Tanzania Afande Sele, ameweka wazi juu ya taarifa iliyoandikwa na wikipedia kwamba aliwahi kuchukua tuzo ya kili music.
Kupitia katika page yake ya Facebook Afande amesema kwamba hajawahi kuchukua tuzo yoyote zaidi ya ile ya Mfalme wa Rhymes, zaidi Afande anasema
Ukisoma historia yangu kupitia WIKIPEDIA kamusi elezo huru, kuna sehemu wameandika kuwa nilishawahi kushinda tuzo za kili wakati si kweli zaidi katika historia yangu yote ya muziki hapa bongo nimeshawahi kushinda tuzo moja tu ya 'KING OF RHYMES' ambayo hata hivyo nilipata kwa kupitia nguvu ya umma tu kwa kuwa 'king of rhymes' ndio shindano pekee katika historia ya muziki wa bongo lililoandaliwa na kuamuliwa kupitia nguvu ya umma kiasi cha kuteka hisia za raia wa rika zote kama ilivyo kwa uchaguzi wa rais.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment