November 22, 2013

NGULI wa muziki wa Bongo Fleva,Seleman Msindi’Afande Sele’ amefunguka kuwa atakapogombea ubunge mwaka 2015 kupitia jimbo la Morogoro Mjini anataka kuwa mbunge wa kwanza kuwa na rasta bungeni.
Akifunguka kupitia kipindi cha mkasi kinachorushwa kupitia EATV alisema kuwa kama katiba ya mwaka haitaruhusu mbunge kufuga rasta hatogombea na kamwe hawezi kunyoa rasta kama atashauriwa anyoe ndio aingie bungeni.
‘’
Kiukweli siwezi kunyoa rasta kama katiba itakataza mbunge kuwa na rasta basi sitagombea ubunge,alisema Afande Sele.
 
Aliongeza kuwa mbona bungeni kuna wabunge wenye asili ya Kihindi(Masingasinga) na wanavaa viremba kwanini yeye asiruhusiwe kuwa na rsta bungeni?alihoji Afande Sele.
'Kiukweli wakazi wa Morogoro wanataka sana niwe mbunge wao kwa kuwa wanajua kuwa najua matatizo wanayowakabili kwakuwa kila siku wananiona nipo nao tangu sijawa staa hadi nimekuwa msanii mkubwa tofauti na wasanii wengine wakishakuwa na majina makubwa wanakimbilia Jijini Dar'alisema Afande Sel

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE