
Mwanaune mmoja aliyedaiwa kuchoma moto chumba cha mzazi mwenzake na kusababisha kifo cha mtoto wa jirani yao huko Mtoni Sabasaba jijini Dar es Salaam na ambaye alitoweka, hatimaye picha yake imepatikana. Katika tukio hilo lililotokea wiki kadhaa zilizopita, mwanaume huyo, Emmanuel Andrea alizozana na mzazi mwenziye, Selina John juu ya mtoto wao mdogo, Tulizo Emmanuel ambapo baba alimtaka mtoto huyo ili asafiri naye kwao mkoani Kilimanjaro.
Akiongea kwa masikitiko akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anapowauguza wanae wengine wawili walioungua katika tukio hilo, Selina alisema siku ya Siku kuu ya Idd mwaka huu, mumewe ambaye pia ni maarufu kwa jina la Mangi, alifika nyumbani na kuhitaji viatu vya mtoto aliyezaa naye.
Selina alisema alikataa kumkabidhi viatu hivyo baada ya awali kupata tetesi kuwa mwenzake huyo alipanga kumtorosha mtoto wao.

huyo ndiye mwanaume aliyedaiwa kuwachoma moto Baada ya muda kidogo, Selina alisema aliamua kuacha shughuli zake na kwenda kumuangalia mtoto wake aliyemkuta amelala dukani kwa mzazi mwenzake na alipotaka kumchukua, likatokea zogo kubwa lililosababisha tukio hilo kufika polisi.
Selina alisema kwa msaada wa majirani zake aliweza kuondoka na mtoto wake na kukimbilia Kituo Kidogo cha Polisi cha Mtongani ili waandikishane na mume wake kama kweli alikuwa na nia njema juu ya kuondoka naye.

mama wa watoto waliochomwa moto
Hata hivyo, baada ya kupigiwa simu na polisi, mwanaume huyo alikataa kufika kituoni. Akiwa bado kituoni hapo, alipata taarifa kwamba chumba chake kinaungua moto huku watoto wake wawili na mmoja wa jirani yao wakiwa ndani.
Watoto wawili waliobakia wanaendelea na matibabu baada ya kuwa wameungua sehemu kubwa ya miili yao, huku mwanaume anayedaiwa kuchoma moto huo akiwa haonekani.
Kutokana na kuwahudumia watoto wake kwa muda mrefu, huku akiwa hana msaada wowote, baada ya vitu vyake vyote kuteketea kwa moto, Selina ameomba msaada kutoka kwa walioguswa na hali yake kwani kwa sasa anaishi kwa msaada wa wasamaria wema na uongozi wa Muhimbili.
Kama kuna mtu aliyeguswa na anahitaji kumsaidia awasiliane naye kupitia namba 0713831702 au 0785845070.
-Gpl
0 MAONI YAKO:
Post a Comment