DAYNA NYANGE
Lea katika ukurasa wake wa facebook mwana dada makali wa bongo freva
anayetamba na wimbo wake wa mimi na wewe, Dayna Naynge ameandika ujumbe
wake wa mwaka mpya na kuaidi kuwasamehe waote walikoseana.
Habari zenu ndugu. Kwanza napenda kumshukuru
mwenyezi mungu anayetupa pumzi bila malipo, kwani yeye ndiyo kila kitu.
Naishkuru familia yangu kwa kunipa moyo kila kukicha mpaka hapa leo hii.
Napenda kutoa shukrani kwenu ndugu zangu kwa kunisapot
katika kazi zangu na ushauli wa kila leo. Tunakutana na mitihani mingi
sana lakini mungu anawapa moyo wa kuwa nami pamoja. shukrani sana kwa
vyombo mbalimbali vya habari kwa mwaka mzima kuendelea kunisapot kwa
kila hali. Radio na Tv mbalimbali kwa kutenga muda wa kupiga nyimbo
zangu na kunipa interview juu ya kazi zangu. nawashkuru sana . Studio
mbalimbali kwa kuweza kunipa nafasi ya kufanya kazi katika studio izo.
Pia Bloggs na website na Magazeti mbalimbali, mmtenga muda wenu kwa
kuthamini kazi za Dayna Nyange mmeonesha ushirikiano mkubwa sana kwangu.
niwashukuru waandaaji wa matamasha kwa kunipa nafasi ya kufanya show
katika matamasha hayo, ni jinsi gani mnavyoonesha kujali kazi zangu na
kunipa moyo. Lakini pia watangazaji na ma dj wa Radio husika mmekuwa
mkitenga muda wa kuwa nami katika kazi zenu,Niwashkuru sana Ma
requester wote Tanzania na nje ya Tanzania kwa ku request nyimbo zangu
na kupata nafasi ya kupigwa katika media izo. Nyinyi ni mchango mkubwa
sana kwa sanaa yetu .Mafans wangu mnaozidi moyo na kunishauli juu ya
kazi zangu na maisha kwa jumla kupitia vyanzo vyangu vya mawasiliano.
Tunafunga mwaka 2013 na tunaamia mwaka 2014 Sitawaangusha.. Mwaka 2013 ,
tumepoteza ndugu zetu tuliokuwa nao ktk tasnia hii. Tuzidi kumuomba
mungu azipumzishe roho zao mahali pema Albert mangwea, Langa kileo, marc
malim Sharomilionea, Sajuki,na wengine wote wapumzike kwa amani.
Nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa wote niliowakosea au kukoseana
kwani ni madhaifu ya kibinaadam. Lakini pia niseme tu kwa wote
walionikosea Nimewasamehe bila kinyongo chochote na kwa dhati toka
moyoni mwangu. Tusahau yaliyopita tuanze mwaka tukiwa Safi. Tumuombe
mungu atupe afya njema na mafanikio zaidi mwaka 2014 na Kuendelea.
Amina.
By
Dayna nyang
By
Dayna nyang
0 MAONI YAKO:
Post a Comment