Muimbaji wa Nigeria, 2face Idibia na mke wake Annie Idibia
wamepata mtoto wa pili – wa kike. Annie Idibia alijifungua mtoto huyo
January 3, 2014 kwenye hospitali ya Atlanta, Georgia, Marekani. Meneja
wake, Naomi Adenuga alithibitisha habari hizo kupitia Twitter. ‘Thank
God for safe delivery …. Princess Idibia is here.”
Wawili hao wana mtoto mwingine mwenye miaka minne aitwaye Isabella.
Hata hivyo 2face hakuwa pamoja na mke wake Marekani kwakuwa alikuwa busy
nchini Nigeria kutumbuiza show za mwisho wa mwaka.
Hadi sasa 2face ana watoto saba, wawili wa kike na mke wake Annie,
wawili wa kiume na mzazi mwenzie Sunmbo Ajaba na wavulana wawili na
msichana mmoja na mzazi mwenzie mwingine Pero Adeniyi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment