Kufuatia kifo cha mtangazaji wa East Africa Radio, Keneth Kidago Lyanga, ona alichosema afande sele
Wkt
huo kituo cha radio(fm) moro kilikuwa kimoja tu nacho ni Ukweli fm
kinachomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la morogoro,kisanii nilikuwa
mchanga sana nikifanya kaz chini ya kaka,rafiki na mwlmu wangu jose
mbilinyi(Sugu),CD zilikuwa ni kitu adimu na chenye thamani sana kiasi
kwamba nyimbo nilizokuwa nashirikishwa na sugu ktk albam zake nyingi
hazikuwa zinapelekwa radioni kama'single'zilikuwa zinabaki
ndani ya albam tu(kanda za casset) ili kusukuma mauzo kwa
mashabiki,lkn kulikuwa na dj/mtangazaji mmoja tu ndani ya radio ukweli
nyakat hizo aliyekuwa ananikubali sana kama msanii wa kwanza kutoka moro
kwenda dar 'kibishi' na kufanya kazi bora kabisa nikiwa na msanii
mkubwa na mkali aliyekuwa anatisha kwa nyakat zile 2 proud,mr 2 baadae
sugu na leo ni mh sugu,huyu dj/mtangazaj alikuwa na kiu kubwa ya kuona
mimi nasikika kwa mashabiki wa nyumbani moro kwa kila hali hivyo akawa
anathubutu kucheza hewani pale redioni zile nyimbo nilizoshirikishwa na
sugu kwa kutumia'Tape'kanda za kaseti'kilazima' na kweli watu
walisikia nami nikasikika ikawa ndio mwanzo wa mimi kukubalika nyumbani
na ugenini,yeye aliitwa keneth kidago lyanga maarufu kama
brother'K',baadae alihamia triple A fm Arusha,nj na mwisho alikuwa est
africa radio akitumikia vipind vya michezo zaid,nina taarifa za kuumiza
sana moyo wangu juu ya mtu huyu,Keny????RiP ndg wa damu!,,,,
R.
I. P Brother k. Tunalia, tutakusahau, lakini mchango wako ni mkubwa
sana kwetu na kwa jamii kwa jumla, nafasi yako itabaki daima. Nakumbuka
wakati upo Radio Ukweli nami nikianza harakati zangu za mziki, uliniahdi
mengi na ulinisaidia sana kwa kiasi
kikubwa mno. Hukuwa na Roho mbaya, ulinijenge na nakumbuka pia wasanii
wengi walikufwata kwa ushauri. Nakumbuka mengi sna kwako. Tangulia
tutaonana nawe muda si mrefu kwani imeandikwa mwanadamu aliyezaliwa na
mwanamke basi siku zake za kuishi wala siyo nyingi. Pumzika pema Brother
K
0 MAONI YAKO:
Post a Comment