Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la
ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti
zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea
zinakabiliana na tatizo hili.
Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia
upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo
hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13.
Pamoja na matatizo mengine kutajwa
kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni
mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye
mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa
masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina
uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi
vifuatavyo:
PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa
kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi
kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa
msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi
wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.
PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho
husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili
linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa
homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko
mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye
utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa
kujamiiana.
NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya
vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo
inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo
ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu
aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.
CHOKOLETI
Ulaji wa Chokoleti huongeza
uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na
mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za
mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita
akiwa mchovu wa mawazo.
CHAZA NA PWEZA
Aina hizi za samaki zinazovuliwa
baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa
vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.
POMEGRANATE
Ni aina fulani ya matunda mekundu
yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na
kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya
tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.
MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na
uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea
mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na
wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.
MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za
matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu
ajione ni mwenye afya njema.
VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa
mwili.
Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na
virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha
kufanya tendo la ndoa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment