Wakazi
wa doma wilayani Mvomero wakiwa mbaroni kwa tuhuma za kufunga barabara
ya Morogoro na Iringa wakishinikiza wafugaji kuondolewa eneo hilo.
WATU 48
wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufunga barabara ya
Morogoro na Iringa wakishinikiza wafugaji wa jamii ya Kimasai kuhamisha
katika eneo la Doma wilayani Mvomero.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Februari 6 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi.
Kamanda
huyo alisema kuwa katika tukio hilo walifanikiwa kuwatia mbaroni
wanawake 24 na wanaume 24 ambao wanadaiwa kufanya vurugu hizo.
Alisema
kuwa fujo hizo zilitokea baada ya watu hao kudai kuwa wafugaji hao
waliwapiga na fimbo wananchi wenzao waliokwenda porini kukata mkaa jambo
lililowafanya nao kuamua kufunga barabara hiyo.
Hata
hivyo kamanda huyo alisema kuwa walifanikiwa kufungua barabara hiyo
majira ya saa 7 mchana baada ya kupiga mabomu ya mchozi kwa lengo la
kuwatawanya wananchi hao.
Alisema kuwa hakuna madhara yeyote ya kibinadamu yaliotokea ingawa watu hao walijaribu kuwapiga mawe polisi hao .
Alisema
kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kwamba watu hao wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani kesho ili kuweza kujibu tuhuma hizo.
Kwa
upande wao wananchi hao wamalalamikia wafugaji hao kitendo chao cha
kuingiza mifugo mashambani na kuharibu mazao njambo ambalo linawarudisha
nyuma kimaendeleo.
Pia
walilalamikia uongozi wa kijiji hicho cha Doma kwa kuwaingiza wafugaji
kinyemela hali inayofanya kuwa wengi huku eneo la malisho likiwa dogo
hali inayofanya wafugaji hao kuingiza mifugo yao mashambani.
Ibrahim
Ndegalo alisema kuwa mbali na wafugaji hao kuwapiga lakini pia wamakuwa
wakiwanyang’anya mali zao bila sabababu na kwamba maisha yao yamekuwa
hayana amani.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment