
THE big
boss wa Kidoti, Jokate Mwegelo ambaye pia ni staa wa sinema na Bongo
Fleva, amefichua siri ya kupatana na Wema Isaac Sepetu akisema kuwa
sababu ya yeye kuonekana kwenye jukwaa moja na aliyekuwa hasimu wake
huyo ni kutafuta amani ya moyo aliyokuwa ameikosa si kweli kwamba
alisukumwa na nguvu ya pombe.
Jokate akicheza sambamba na Wema ndani ya Ukumbi wa Triple A, Arusha.
Wawili hao walipatana hivi karibuni wakiwa jijini Arusha.
Akizungumza na gazeti namba
moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Jokate alisema ilipokaribia
siku ya kwenda Arusha, Wema alimkaribisha kwenye shoo yake iliyofanyika
jijini humo lakini alimwambia kuwa amebanwa ila akamuahidi kwamba
akimaliza mambo yake atakwenda kumsapoti.
“Wema
aliondoka bila kujua kama nitakwenda lakini nilipopanga ratiba yangu
ikakaa sawa, niliamua kwenda na kumfanyia ‘sapraizi’ na si kweli kwamba
nilisukumwa na nguvu ya pombe,” alisema Jokate.
Jokate
alisema kwamba hakushauriwa wala kujadiliana na mtu yeyote isipokuwa
aliamua mwenyewe kufanya jambo hilo ambalo lilikuwa likimkosesha faraja
kwa muda mrefu.
“Nimeamua
kumaliza mabifu kwa sababu nilikosa amani ninayoitaka kwa muda mrefu.
Ukweli Wema alinikaribisha, nikaona ndiyo sehemu ya kutimiza lengo langu
la kupatana naye,” alisema Jokate ambaye aliingia kwenye gogoro na Wema
baada ya kutembea na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment