
Katika kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali barabarani wakali katika muziki wa bongo fleva Mr Blue, Amini, Barnaba Boy na Dyna Nyange wameshiriki kurekodi wimbo wao utakaotumika kwenye kampeni ya dereva makini inayolenga kuhamasisha uzingatiaji wa usalama barabarani na kwenye vyombo vya usafiri. Wimbo huo umerekodiwa na mtayarishaji wa muziki C9.
Kampeni hiyo ya dereva makini imeandaliwa na Transevents Marketing kwa lengo la kutoa hamasa kwa madereva kuwa makini wanapoendesha magari ili kuwawezesha abiria kufika salama waendako.
Audio ya wimbo wa dereva makini imesharekodiwa na kinachosubiriwa ni video yake, tazama video ya maelezo ukitumia link hii hapa chini.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment