April 11, 2014

Beki Kelvin Yondani hajulikani alipo, uongozi haujui na hata benchi la ufundi halitaki kulizungumzia suala Lake. Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa amesema hajui lolote kuhusiana na beki huyo na asingependa kuzungumzia.

“Sina taarifa yoyote kuhusiana na na Yondani,” alisema.

Lakini alipoulizwa bosi wake, Hans ven der Pluijm, naye alisema anachofanya ni kufanya wachezaji waliopo.

“Sasa nisingependa kumzungumzia Yondani, waliopo ndiyo ninafanya nao kazi na nguvu tunaelekeza katika mechi zilizobaki na tunataka kushinda zote,” alisema.

Viongozi wamekuwa wakikwepa kulizungumzia, lakini Yondani inaelezwa aliondoka mara tu baada ya mechi ya Mgambo ambayo Yanga ililala kwa mabao 2-1 mjini Tanga.

Rafiki wa karibu wa Yondani, amesema kwamba, beki huyo alikasirishwa na kuvishwa lawama alizoona hazikuwa na msingi, kwamba alihujumu kwa kuwa alisababisha penalty iliyozaa bao la pili.

“Unajua yeye ni beki, kosa linaweza kutokea na anaona anaonewa bila sababu za msingi na mbaya kuna baadhi ya viongozi wanaonekana kuungana na wale wasiojua mpira na kusisitiza alisababisha penalty kwa makusudi.

“Sasa hali hiyo imemuudhi na ukizingatia alicheza kwa nguvu sana, alijituma sana siku ile kwa kuwa anajua umuhimu wa ubingwa,” alisema rafiki yake huyo wa karibu bila ya kusema Yondani amejijimbia wapi.

Kabla ya kujiunga na Yanga, wakati huo akiwa Simba, Yondani alikimbilia kwao Mwanza na kujichimbia chanzo likiwa suala la lawama na kushutumiwa kuwa aliifungisha Simba makusudi.

Source:udakuspecially.com

Related Posts:

  • Mwandishi wa habari ashtakiwaMwandishi mmoja wa habari mashuhuri ambaye pia ni mkereketwa wa haki za kibinadamu amefikishwa mahakamani nchini Angola kwa mada Mwandishi mmoja wa habari mashuhuri ambaye pia ni mkereketwa wa haki za kibinadamu amefikishwa m… Read More
  • Nay wa Mitego achukua maamuzi magumu kuhusu mtoto Nay wa Mitego na Mtoto wakeNay wa Mitego Amesikitishwa na Kauli ya Mzazi mwenzake SIWEMA ambaye wamezaa naye mtoto kwa kusema kuwa mtoto huyo si wa kwake bali ni wa aliyekuwa  Mpenzi wake wa zamani Obasanjo...Japo Wahen… Read More
  • Magazeti ya leo hii March 26 haya hapa Leo Alhamisi Tarehe 26 March 2015. Tunakupatia fursa ya kutembelea kurasa za magazeti ya leo hii kama tulivyoyapata … Read More
  • CUF waitaka tume ya Taifa kukili kushindikana kwa kura ya maoni Naibu mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho ABDUAL KAMBAYA akizngumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam kuhusu mchakato mzima wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa kielecron… Read More
  • England kuandaa kombe la dunia  Sepp Blatter Rais wa FIFA England sasa inafikiria kuingia katika kinyanganyiro cha kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2026 baada ya kujaribu bahati hiyo ilii iandae fainali hizo mwaka 2018 lakini ilijikut… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE