MWILI wa mwimbaji mahiri nchini aliyefariki dunia wiki iliyopita nchini Thailand, Amina Ngaluma ‘Japanese’ umewasili jijini Dar es Salaam jana usiku huu.
Nyota huyo wa
zamani wa bendi mbalimbali nchini ikiwamo Double M Sound, African
Revolution ‘Wana Tamtam’, mpaka mauti yanamfika alikuwa mwanamuziki wa
bendi ya Jambo Survivors.
Kwa mujibu wa
mume wa marehemu, Rashid Sumuni, msiba upo kwa wazazi wa marehemu
Kitunda, Machimbo, Dar es Salaam ambako ndiko maziko yatafanyika hapo
kesho mchana.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMINA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
0 MAONI YAKO:
Post a Comment