1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
1. Vanessa Mdee – Choice FM
2. Millard Ayo – Clouds FM
3. Hamis Mandi aka B12 – Clouds FM
4. Mariam Kitosi – Times FM
5.Ergon Elly – Mbeya Highlands FM
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
1. The Hitlist – Choice FM
2. Xxl – Clouds FM
3. Amplifaya – Clouds FM
4. Hatua Tatu – Times FM
5. Power Breakfast- Clouds FM
3. MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
1. Salama Jabir - EATV
2. Sam Misago - EATV
3. Zamaradi Mketema- Clouds TV
4. Salim Kikeke – BBC Swahili
5. Gondwin Gondwe – ITV
4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
1. Friday Night Live – EATV
2. Mkasi – EATV
3. Planet Bongo - EATV
4. Uswazi - EATV
5. Take One – Clouds TV
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
1. Juma Kaseja – Yanga
2. Mrisho Ngassa – Yanga
3. Mbwana Samatta – TP Mazembe
4. Ramadhan Singano – Simba SC
5. Francis Cheka
6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
1. Nisher
2. Adam Juma
3. Nick Dizzo
4. Mecky Kaloka
5. Jerry Mushala
7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
1. My Number - Diamond
2. Jikubali – Ben Pol
3. Mirror – Baby
4. Love Me - Izzo Bizness f/ Barnaba & Shaa
5. Muziki Gani - Nay wa Mitego f/ Diamond
8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
1. Amani ya Moyo – Feza Kessy
2. Closer – Vanessa Mdee
3. Sugua Gaga – Shaa
4. Yahaya – Lady Jaydee
5. Nakomaa na JIJI - Shilole
9. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
1. Elizabeth ‘Lulu’ Michael
2. Jacqueline Wolper
3. Shamsa Ford
4. Irene Uwoya
5. Wastara Juma
10. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
1. Jacob Stephen aka JB
2. King Majuto
3. Vincent ‘Ray’ Kigosi
4. Hemedy Suleiman
5. Salim ‘Gabo’ Ahmed
11. FILAMU INAYOPENDWA
1. Foolish Age – Elizabeth Michael
2. Bado Natafuta – Salim Ahmed, Shamsa Ford
3. Shikamoo Mzee – JB, Shamsa Ford, Majuto
4. Ndoa Yangu – Kanumba, Wolper
5. Zawadi Yangu – JB, Irene Uwoya
Akizungumzia tuzo hizo, meneja habari wa Bongo5, Fredrick Bundala
amesema,"Upigaji kura utaendelea na sasa utajikita tu katika orodha ya
majina haya matano, yaliyotangazwa kuongoza kwa kura, kwenye kila
kipengele kinachoshindanishwa".
Wiki moja baada ya majina ya washiriki watano kutangazwa, mchujo wa
kwanza utafanyika katika kila kipengele na kati ya wanaowania, mmoja
ataondolewa na kubakiza wanne.
Wiki moja baada ya mchujo huo wa kwanza, mchujo wa pili utafanyika na kuwabakiza wanaowania watatu kwenye kila kipengele.
Wanaowania tuzo wote (watatu katika kila kipengele) waliosalia baada ya
kufanyika mchujo wa pili na (wa mwisho), watakuwa wageni wa heshima
kwenye utoaji wa tuzo hizo, utakaofanyika wiki mbili baada ya mchujo huo
wa pili, ili kutoa nafasi ya mashabiki wao kuendelea kupiga kura.”
Tunawaomba WaTanzania waendelee kuwapiga kura kupitia tovuti yetu,
www.tuzozetu.com na pia kwa kutuma ujumbe mfupi wa neno TUZOkwenda 15678
na baadaye kufuata maelekezo rahisi ya kupiga kura, alisema Fred.
KUHUSU TUZO ZA WATU 2014
Tuzo za watu Tanzania ni tuzo za aina yake, zilizoanzishwa kwa mara ya
kwanza nchini mahsusi kwaajili ya kuwapa mashabiki wa muziki, filamu,
michezo na burudani, jukwaa huru kuwachagua wanaowapenda na kuwakubali
katika vipengele vinavyoainishwa na tuzo hizi.
Tuzo hizi zitakazokua za kwanza kwa mwaka 2014, zinatarajiwa kuendeshwa kila mwaka.
Tuzo za watu zinalenga kuanzisha mchakato wa wazi na huru wa utambuzi
wa watu wenye umuhimu na michango mahsusi katika nyanja
mbalimbali,wanaochaguliwa moja kwa moja na wananchi wenyewe. Tuzo hizi
zitatumika kuanzisha urithi utakaoleta hatua mpya ya heshima kwenye
jamii yetu
0 MAONI YAKO:
Post a Comment