Msimamizi wa Nyumba hiyo akimuonyesha
Mwandishi wetu Uvungu aliofichwa mtoto huyo
Msimamizi huyo akitoka nje ya nyumba
hiyo na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa kijiji hicho akihojiwa na mwandishi wetu
Dustans Shekidele mwandishio wa habari hii

Mtoto Devota akikunja sura kwa uchungu wa maumivu

Muuguzi akimfunga kidonda Devota
Na Dustans Shekidele,Morogoro.
SAKATA la
mtoto Devota Malole mwenye umri wa miaka 5 ambaye ni mlemavu
aliyeibuliwa baada ya kufichwa chini ya uvungu wa kitanda kwa muda wa
miezi mitatu huko Matongolo, Dumila,Tarafa ya Magole wilayani Kilosa
limeibua mambo mapya, baada ya kubaini kuwa aliyesababisha kuokolewa ni
mume wa mama wa binti huyo.
Mashuhuda waliokuwepo wakati wa kufichuliwa kwa mtoto huyo, wakiwemo
majirani na wapangaji wa nyumba aliyokuwa akiishi, walisema mpangaji wa
chumba hicho, Masumbuko Mkwama (25), aliishi peke yake kwa muda mrefu
kabla ya miezi mitatu iliyopita, kuja na mwanamke aliyemzidi umri, Salah
Mazengo (36) aliyemtambulisha kama mke wake akiwa na watoto watatu.
Msimamizi wa nyumba hiyo, Donata Sisie ambaye alidai mwenye nyumba
anaishi Morogoro mjini, alisema baada ya kumuhoji mwanamke huyo, alisema
alikuwa na watoto watano na kila mmoja alikuwa na baba yake na kwamba
watatu kati yao, walichukuliwa na wazazi wao na hivyo kubaki na wawili,
Elias mwenye umri wa miaka nane na mdogo wa mgongoni.
“Juzi Julai 8, Masumbuko aliwafuata wapangaji wenzake watatu na
kuwaeleza kwamba mkewe ana mtoto mlemavu ambaye ni mgonjwa, lakini
mwanamke huyo hataki mwanaye atibiwe, jambo ambalo linamshangaza. Kwa
pamoja, watu hao walikwenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji,
ambaye baada ya kuelezwa juu ya mtoto huyo, aliamua kwenda polisi.
“Julai 10, mwaka huu, askari polisi pamoja na mwenyekiti huyo walikuja
hapa nyumbani na kumfichua mtoto huyo chini ya uvungu. Tokea siku ya
tukio, Masumbuko hajulikani alipo.
“Juzi ulitokea mvutano mkali hapa kwani mama mzazi wa Sala alifika
akitaka kuchukuwa vyombo vilivyomo ndani ya chumba cha Masumbuko, mimi
nilimzuia kwa hoja kwamba ninachojua chumba ni cha mvulana hivyo
nimevichukua vitu vyake na kuvihifadhi kwangu hadi atakapofika.”
Mmoja wa wapangaji wenzake na Masumbuko, Asha Mohamed alisema alipohamia
yeye na mumewe, walimkuta Masumbuko akiishi peke yake hadi miezi mitatu
iliyopita walipomuona akimleta mwanamke mtu mzima aliyekuwa na watoto
watatu, mmoja akiwa na ulemavu wa miguu.
Alisema alimuona mtoto mlemavu akiwa salama kwa siku moja tu, ile aliyofika na tangu hapo hakumuona tena.
“Alipokuja alikaa naye hapa kwenye korido, sijamuona tena hadi juzi
alipofichuliwa akiwa tofauti na nilivyomuona mwanzo, kiukweli huyo mtoto
alizaliwa akiwa mlemavu na kwa mujibu wa maelezo ya mama yake, baba
yake alimkana baada ya kumuona na ulemavu.
“Niwe mkweli kwenye hili, mtoto huyu alifichwa uvunguni tangu ahamie
hapa, hii inatokana pengine na ugumu wa maisha kwani kwenye chumba chao
wana kitanda futi nne na wanalala wanne baba, mama mtoto wao mkubwa
Elias na huyo mtoto wa mgongoni, kuna kipindi nilimuuliza Devota alikuwa
wapi aliniambia kuwa alimpeleka kwa bibi yake yaani mama yake anayeishi
kitongoji kinachofuata,” alisema Asha.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa kitongoji hicho, Dotto Hambosi alisema
baada ya kupewa taarifa na wananchi wake aliwasiliana na polisi, ambao
kesho yake walifika na kumkamata mwanamke huyo baada ya kukiri kuwa na
mtoto uvunguni mwa kitanda chake. Baadaye walimpeleka Kituo cha Polisi
Dumila kabla ya kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa
anakopatiwa matibabu.
Juu ya kazi za wazazi hao wawili, Hambosi alisema mwanaume anauza
mishikaki na mwanamke pombe za kienyeji katika kilabu cha pombe za
kienyeji.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment