July 15, 2014

Wapalestina wakusanyika kuona kombora lililorushwa kutoka Israel

Mashambulizi ya angani yanayofanywa na Israel katika eneo la Gaza yameendelea huku oparesheni ya Isreal dhidi ya wapiganaji wa kipalestina ikiingia siku yake ya 7.
Mashambulizi hayo yakiendelea, wapiganaji wa kipalestina nao wamekuwa wakirusha makombora ndani ya Israel.
Maafisa wa Palestina wanasema kuwa takriban watu 172 wameuawa tangu mashambulizi hayo yaanze jumanne iliopita.
Israel inasema kuwa takriban makombora 1000 ya roketi yamerushwa kutoka Gaza katika mda huo.
Imesema kuwa iliidungua ndege moja ya Palestina isiyo na rubani karibu na eneo la Ashdod hii leo asubuhi.
Awali maelfu ya raia walitoroka kutoka Kaskazini mwa Gaza kufuatia onyo la israel.
Israel na Palestina zimekuwa zikipigana kwa siku saba sasa tangu mgogoro huu mpya kuanza
Jeshi la Israel liliangusha vijikaratasi katika mji wa Beit Lahiya likionya kuhusu mashambulizi zaidi.
Israel imeweka maelfu ya wanajeshi wake katika mpaka na Gaza huku ikitishia kutekeleza uvamizi wa ardhini.
Makomando wa Israel walitekeleza mashambulizi yao ya kwanza ardhini siku ya jumapili,ambapo walikishambulia kituo kimoja cha kurusha makombora ya roketi.
Mawaziri wa maswala ya kigeni kutoka mataifa ya kiarabu wanatarajiwa kukutana mjini Cairo hii leo ili kujuadiliana kuhusu mgogoro huo huku idadi ya waathiriwa ikiongezeka.
Umoja wa mataifa unakadiria kwamba asilimia 77 ya watu waliouawa katika eneo la Gaza ni raia.
Hata hivyo msemaji wa jeshi la Israel Luteni kanali Peter Lerner amekosoa idadi hiyo akisema hi kulinga na duru za hamas na kwamba hazina ukweli wowote.
Kanali Lerner amesema kuwa israel ilisitisha baadhi ya mashambulizi yake kwa hofu ya kuwauwa raia.

Related Posts:

  • Anayetuhumiwa kumtukana Rais Magufuli amepata dhamana     Baada ya Mahakama ya hakimu mfawidhi Arusha kukaa chini na kupitia hoja mbili zilizotolewa na upandea wa mashtaka na mshitakiwa Mahakama imeridhwa ia kutoa dhamana … Read More
  • Karibu katika Magazeti ya leo Jumatatu April 18     Habari za leo hii jumatatu ya 18 April 2016. Karibu mpendwa katika kurasa za magazetini leo hii. Tumekuwekea kurasa zilizobeba uzito katika magazeti ya leo jhii. Kupata habari kwa undani fika katika meza za … Read More
  • Baby Madaha kuja na Corazon Msanii wa muziki na mwigizaji, Baby Joseph Madaha, ‘Baby Madaha’ baada ya ukimya wa muda mrefu amejipanga kuachia wimbo wake mpya ‘Corazon’. Madaha amesema kwa sasa anamalizia video ya wimbo huo ambao picha zake … Read More
  • Muuaji aua watu 182   Waziri wa mawasiliano Getachew Reda Wananchi wa Ethiopia wameeleza namna muuaji wa watu zaidi ya 182 kuwa alikuwa ameshikilia bunduki na ni raia wa Sudan Kusini upande wa Magharibi mwa Gambela mk… Read More
  • Zifahamu siri saba za ‘smartphone’ ambazo hukuzifahamu MATUMIZI ya simu za kisasa (smartphone) yamezua maneno na uvumi wa kila aina katika blogu, magazeti mbalimbali, barua-pepe, mitandao ya WhatsApp na Facebook, hata hivyo, mtumizi wa simu hizi hatakiwi kua… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE