Juventus
na Roma wanataka kumsajili beki wa kati wa Manchester City Matija
Nastasic, 21, huku Newcastle na West Ham wakimtaka beki wa kulia wa Man
City Micah Richards, 26, (Manchester Evening News), Manchester United
wanaongoza mbio za kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 26
baada ya mabingwa wa Ufaransa PSG kuamua kujitoa (Daily Star), lakini Di
Maria huenda asiende United kwa sababu Louis van Gaal hataki kukwaza
ukuaji wa Adnan Januzaj, 19, (Daily Express), Tottenham wanajiandaa
kutoa pauni milioni 11 kumchukua mshambuliaji wa QPR Loic Remy, 27,
(Daily Star), Arsenal wanafikiria kupanda dau kumchukua beki wa West Ham
Winston Reid, 26, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao (Daily
Star), Hull City wameongeza dau kumchukua mshambuliaji wa Blackburn
Jordan Rhodes, 24 (Daily Mail), kiungo wa Manchester United Anderson,
26, huenda akahamia Sporting Lisbon kwa pauni milioni 5.5 (Daily
Express), boss wa Southampton Ronald Koeman amesema kiungo wake Morgan
Schneiderlin, 24 hauzwi kwa bei yoyote (London Evening Standard), beki
wa QPR Rio Ferdinand, 35, anataka kuwa meneja wa England akistaafu
kucheza (Daily Mail), Newcastle United wana uhakika nahodha wao msaidizi
Cheick Tiote, 28 hatoondoka licha ya timu nyingi kumnyatia (Sunderland
Echo), boss wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Jack Wilshere, 22,
anatolewa kafara kwa England kushindwa kufanya vizuri katika Kombe la
Dunia (Sun), wakati huohuo Aaron Ramsey, 23, ana uhakika Arsenal
wataweza kupambana "kwa misuli" na Manchester City na Chelsea msimu huu
(Sky Sports), Barcelona wamefanya jaribio la kushangaza la kumtaka Angel
Di Maria kutoka Real Madrid. Real walifikiria dau la pauni milioni 48
lakini mazungumzo ya awali yalivunjika baada ya Los Bloncos kutotaka
kuwauzia mahasimu wao (Sport), Napoli wanamtazama Fabio Borini wa
Liverpool, ambaye kuwasili kwa Mario Balotelli huenda kukasaidia
kufanikisha uhamisho wake (Tuttosport), dau la Manchester United kumtaka
Nicolas Gaitan limekataliwa na Benfica (Record), Arsenal wanafikiria
kumchukua William Carvalho kutoka Sporting, huku Sami Khedira anaweza
kwenda Emirates iwapo atashusha madai ya mshahara mkubwa (Daily
Telegraph), AC Milan wanajiandaa kumtaka mshambuliaji wa Tottenham
Roberto Soldado kuziba pengo la Mario Balotelli anayeelekea Liverpool.
Spurs watamruhusu Soldado kuondoka na nafasi yake kuzibwa na Loic Remy
kutoka QPR (Daily Mail), Manchester United na Zenit St Petersburg wapo
tayari kupambana kumwania kiungo wa Inter Milan Fredy Guarin (Corriere
dello Sport), Barcelona wanatumaini kukamilisha usajili wa Marco Reus
kutoka Bayern Munich.
Maafisa wa Bayern wana wasiwasi kuwa huenda mchezaji huyo tayari
amekubali kujiunga na Catalans ambao huenda wakafungiwa kusajili (Mundo
Deportivo). Zimesalia siku 10 kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.. |
0 MAONI YAKO:
Post a Comment