September 23, 2014

Screen Shot 2014-09-23 at 9.00.34 AM 
Yupo kwenye orodha ya Wasanii ambao wanazo rekodi zao kwenye chati ya muziki wa bongofleva Tanzania na nchi jirani zinazocheza muziki wa kiswahili ambapo baada ya miaka kadhaa ya kuifanya bongofleva aliamua kuhamia Kenya kutafuta mkwanja zaidi pia kuuongezea muziki wake ladha nyingine.
Sasa hivi ataonekana sana kwenye kioo chako baada ya kutoa hii video mpya aliyoifanya Kigali Rwanda ambapo jina la video lilikua liwe ‘nimepona’ ila jamaa wakakosea na kuiandika ‘mimi na wewe’ ila sio kesi.
Screen Shot 2014-09-23 at 8.59.10 AM 
Hussein Machozi amesema alipata nafasi ya kuifanya video hii kwenye nyumba ya Rais Paul Kagame kirahisi sababu producer wa hii single ni Mrwanda na hata yeye mwenyewe Hussein ana asili ya Rwanda kwa upande wa mama mzazi, hivyo vyote vimesaidia kwake kupata nafasi hiyo.
Rais Paul Kagame ambae ni miongoni mwa Marais wanaopenda sana kuwasaidia vijana ambae pia ana rekodi za kusaidia hata Wasanii wa nchi yake, huwa haishi kwenye hii nyumba bali familia yake.
President Kagame aliwahi pia kumsaidia mmoja kati ya Wasanii vijana wa Rwanda lakini mwaka huu msanii huyo ameingia kwenye kashfa ya kutaka kuipindua nchi ikiwemo kumpindua madarakani Rais Paul Kagame mwenyewe.
Screen Shot 2014-09-23 at 8.59.22 AM 

Related Posts:

  • Mbowe Anyang'anywa Gari Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimesikitishwa na hatua ya uongozi wa Bunge la Tanzania ya kulichukua gari la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe alilokuwa akilitumia kwa sh… Read More
  • Watanzania hawatatuelewa - Mwakyembe   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa endapo watashindwa kufanya maandalizi mazuri ya michuano ya mataifa ya Africa (AFCON) kwa vijana 2019 basi Watanzani… Read More
  • Ancelotti atimuliwa Bayern   Kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti amefutwa kazi leo kufuatia mwanzo mgumu wa msimu wa 2017/18 yakiwemo matokeo ya jana usiku ambapo timu hiyo ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa PSG. Mkurugenzi … Read More
  • Breking News: Mbunge Pete Msigwa akamatwa na Polisi   Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa (Chadema) amekamatwa na polisi leo Jumapili jioni baada ya kushushwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlandege mkoani Iringa. Mwenyekiti wa Baraza la Vijana … Read More
  • Daktari aeleza hatari ya vyuma vilivyoko kwenye moyo wa Manji   Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mustapha Bapumia (62) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anashangaa mtu mwenye umri mdogo kama Yusufali Manji (41) kuw… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE