
Afande Sele baba tunda akiiwakilisha Morogoro vizuri sana
Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 linaloendelea kuzunguka mikoa mbalimbali, siku ya jana wakazi wa Mji kasoro Morogoro ilikuwa zamu yao sasa pale walipopata fursa ya kushuhudia burudani kabambe ya wasanii kibao katika Stage moja. Mambo yalikuwa hivi

Wasanii
wa muziki wa kizazi kipya Stamina na Ney wa Mitego wakilishambulia
jukwaa mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Morogoro mapema jana ndani ya
uwanja wa Jamhuri.Huko kwenu vp??
.jpg)
Msanii
wa Bongo Fleva Vanessa Mdee a.k.a V-Money akitumbuiza mashabiki
waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwenye Tamasha la
Fiesta 2014.

Mmoja wa mashabiki aliyekuwa kwenye Tamasha la Fiesta akishangilia huku akiwa amebebwa na mwenzake.

Vanessa Mdee akipagawisha jukwaani.
Daudi wa kota na Adam Mchomvu wakiwa Back Stage



Umati uliyokuwa umefurika kwenye Tamasha la Fiesta 2014, ukishangilia
moja ya burudani zilizokuwa zikitolewa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.

Mashabiki wakishangweka

Makomando wakiwajibika jukwaani hapo.

Ommy Dimpoz akiimba na mmoja wa mashabiki aliyekuwa akiimba kwenye nafasi ya Vanessa Mdee katika wimbo wa Me & U.

Msanii wa kike Linah wa kwanza kutoka kushoto akiwajibika jukwaani na mmoja wa wanenguaji wake.

Chipukizi wa Bongo Fleva Mo Music akikamua kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta mjini Morogoro, usiku wa kuamkia leo.

Mmoja
wa mashabiki akiwa amebebwa jujuu wakati shangwe za Serengeti Fiesta
2014 zikiendelea usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.

Fid Q akifanya yake kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mashabiki wakishangilia

Baba Levo na Peter Msechu wakipagawisha jukwaani hapo

Kundi la Weusi kutoka nyanda za Kaskazini wakifanya makamuzi yao kwenye jukwaa la Fiesta, usiku wa kuamkia leo mjini Morogoro.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment