
MSANII
wa muziki wa hip hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ anaendelea
kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukamatwa na dawa za
kulevya na kesho anatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Chidi
Benzi alikamatwa na dawa za kulevya juzi jioni katika Uwanja wa
Kimataifa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam wakatia wa ukaguzi kabla
ya kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa Kamanda wa
Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Alfred Nzowa,
msanii huyo ameendelea kushikiliwa na jeshi la polisi mpaka kesho
atakapofikishwa mahakamani.
Alisema Chidi Benz
alikamatwa na dawa aina ya Heroine kete 14 na misokoto miwili ya bangi,
vyote alikuwa ameiweka katika mfuko wa shati alilokuwa amevaa.
“Dawa alizokamatwa nazo
zilikuwa kwa ajili ya matumizi yake, jeshi limeendelea kumshikiria mpaka
Jumatatu kwa sababu leo (jana) na kesho (leo) sio siku za kazi,”
alisema.
Mbali ya dawa, msanii
huyo alikutwa katika begi yake na kigae kidogo cha chungu na kijiko,
ikiwa ni maandalizi ya kutumia dawa hizo.
Msanii huyo alikuwa
anakwenda jijini Mbeya kwa shoo ya ‘Instagram Party’ iliyofanyika jana
katika ukumbi wa City Pub, jijini humo.
Chidi Benzi alikuwa
ameongozana na msanii mwenzake Nurdin Bilal ‘Shetta’ ambaye naye
alishikiliwa kwa muda kabla ya kuachiliwa kuendelea na safari yake
0 MAONI YAKO:
Post a Comment