
Ni
miezi sita sasa baada ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram
kuwateka wanafunzi wasichana Zaidi ya 200 kaskazini mashariki mwa
Nigeria, wasichana watatu ambao wametoroka wamezungumza katika mahojiano
maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC.
Tukio
hili linakuja wakati serikali ya Nigeria ikiwa katika makubaliano ya
kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram hatua itakayosaidia kuwaachilia
huru wasichana waliotekwa na kundi hilo.
'' nilikuwa nataka
kurukia nje wakati msichana mwenzangu aliponikamata kwa nyuma na kusema
watakupiga risasi kama utafanya hivyo. Nikasema, nini utofauti wataniua
mimi hapa na kuacha maiti yangu ikusachukuliwa nilikuwa nalia na kuomba
mpaka tulipoifikia kambini" Anasimulia msichana mmoja aliyetoroka
mikononi mwa Boko Haram.
Akizungumza katika
mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC, Msichana huyu anakumbuka
jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori wakati wapiganaji wa Boko Haramu
walipomteka yeye na wasichana wengine.
Zaidi ya wasichana 200
kati miongoni mwao walikuwa walitekwa lakini wale waliokimbia
walibahatika kutoingia katika hofu kubwa kwenye mikono ya watekaji.
Shirika la kimataifa la
kutetea haki za binaadam la Human Rights Watch limesema wanawake
wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haramu wamekuwa wakinyanyaswa, kubakwa
na hata kulazimishwa kuolewa.
Katika ripoti mpya ya
shirika hilo inasema Wanamgambo hao wa Kiislam wamewawateka wanawake
Zaidi ya 500 na wasichana tangu mwaka 2009.
Serikali ya Nigeria hivi
karibuni imetangaza makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko
Haram ambayo hatua itakayawafanya wanamgambo ho kuachilia huru wasichana
hao waliotekwa huko Chibok.
Lakini Boko Haram wenyewe
hawajawahi kuthibitisha makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano na
hakuna dalili zozote za kuachiwa kwa wasichana hao hivi karibuni.
Lakini kwa wale waliobahatika kutoroka, matatizo ya kisaikolojia bado yanawasumbua
0 MAONI YAKO:
Post a Comment