
DR. Dree akivalia vipaza sauti vya Beat
Wasanii mashuhuri wa Marekani Dr Dre na Jimmy Loving wanashtakiwa na
mshirika wao wa kibiashara ambaye waliunda naye vipaza sauti vya
masikioni ama headphones kwa jina Beats Headphone range.
Noel Lee ambaye kampuni yake Monster ilisaidia kuzindua vipaza sauti
hivyo vya Dr.Dre mnamo mwaka 2008,anasema kuwa kampuni yake ilisalitiwa
na teknologia yake kuibwa.

DR. Dree
Anadai kwamba alipoteza mamilioni baada ya msanii Dre na Jimmy Iovine
walithibiti visivyo vipaza sauti hivyo kupitia udanganyifu.
Baada ya kukata uhusiano wake na Monster,Beats ilinunuliwa na Apple kwa dola billioni 3.
Katika nakala za kesi hiyo zilizowasilishwa katika mahakama ya
Carlifonia,Lee anadai msanii huyo wa muziki wa rap Dr Dre hakuhusika
pakubwa katika kutengeza vipaza sauti hivyo vilivyo na jina lake.
DR.Dree akiwa na wenzake
Lakini vipaza sauti hivyo vilipata umaarufu mkubwa na kuanza kutumiwa na
watu mashuhuri na mashabiki wa muziki huku ushawishi wa Dr Dre ukifanya
biashara hiyo kufaulu.
Hakuna tamko lolote kutoka kwa wakili wa Dr Dre ama kutoka kwa beats.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment