January 30, 2015

Rais Barack Obama anatarajiwa kuzindua bajeti yake ya mwaka 2016, jumatatu 
Rais Barack Obama anatarajiwa kuzindua bajeti yake ya mwaka 2016, jumatatu
White House ilisema Rais Barack Obama anaangalia kumaliza “enzi ya matatizo ya kutengenezwa  na kubana matumizi bila ya sababu za msingi” wakati akipanga kuzindua mpango wake wa matumizi ya serikali mwaka 2016.
Katika taarifa ya alhamis White House ilisema bwana Obama, m-Democrat atatoa wito wa kuondoa makato ya  moja kwa moja  ya matumizi ambapo alikubaliana na wabunge wa upinzani wa Republican wakati wa matatizo ya bajeti mwaka 2011 wakati Marekani ikitaabika kuondoka katika hali ya kudorora kwa uchumi duniani.
Pendekezo la bwana Obama kwa bajeti ya  mwaka 2016 lililopangwa kutolewa jumatatu litatoa wito kwa asilimia saba ya nyongeza ya matumizi—dola bilioni 74 juu ya kile vyama vya siasa walivyokubaliana hapo awali. White House ilisema makato ya moja kwa moja ya matumizi yanayojulikana mjini Washington kama “hatua za kisheria za kuzuia mali hadi deni lilipwe” imeumiza uchumi wa Marekani na jeshi lake.
                                                                           Rais Barack Obama       Rais Barack Obama

Bwana Obama na White House wanataka “kubadili kikamilifu”  makato katika matumizi ya ndani wakati ikitoa nyongeza sawa ya matumizi kuboresha  program za jeshi na usalama wa taifa. Mpango wa bajeti kwa mwaka unaanza mwezi Oktoba utatoa wito wa nyongeza ya matumizi kwa ujenzi wa viwanda, barabara na madaraja na ulilenga utafiti wa huduma ya afya kwa tiba ya kisukari na saratani.
Pia itajumuisha wito kwa viwango vilivyolenga kwenye kusaidia watu wa daraja la kati nchini Marekani kwa kuwapatia punguzo la kodi kwa huduma ya mtoto, kulipwa likizo ya ugonjwa na miaka miwili ya kufadhili masomo  kwa wanafunzi wa vyuo vya kijamii. 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE