Federica Mogherini
Umoja wa Ulaya umezitaka pande zote zinazozozana huko Misri kudumisha amani nchini humo. Federica Mogherini
mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya ameashiria utumiaji nguvu za
ziada na kuuawa raia kadhaa wa Misri katika mapigano ya hivi karibuni na
kusisitiza juu ya ulazima wa kufanyika kwa amani maandamano nchini
humo.
Mogherini amezitaka pande zote zinazozozana huko Misri kufanya
mazungumzo kama njia pekee itakayoweza kutatua mgogoro wa nchi hiyo na
kudumisha amani nchini. Mikoa na miji mbalimbali ya Misri jana
ilishuhudia mapigano na utumiaji mabavu katika kuadhimisha mwaka wa nne
tangu kujiri mapinduzi ya wananchi ya tarehe 25 Januari yaliyomng’oa
madarakni dikteta wa nchi hiyo Hosni Mubarak mwaka 2011. Watu zaidi ya
20 wakiwemo polisi watatu waliuawa jana wengine 82 kujeruhiwa katika
vurugu za jana huko Misri.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment