Armel Mingatoloum Sayo, Waziri wa Vijana, Michezo, Sanaa na Utamaduni wa CAR aliyetekwa nyara na magaidi wa Anti-Balaka
Watu wanaosadikiwa kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Anti-Balaka la
Jamhuri ya Afrika ya Kati wamemtaka nyara Waziri wa Vijana, Michezo,
Sanaa na Utamaduni wa nchi hiyo. Nicaise Danielle Sayo mke wa waziri
aliyetekwa nyara na magaidi wa Anti-Balaka amesema kwamba, tukio hilo
lilitokea wakati yeye na mumewe walipokuwa wakirejea nyumbani wakitokea
kanisani, ambapo watu wasiojulikana walipomteka nyara mumewe katika eneo
la Galabadja jirani na mji mkuu Bangui. Taarifa zaidi zinasema, baada
ya Anti-Balaka kumteka nyara Armel Mingatoloum Sayo, Waziri wa Vijana,
Michezo, Sanaa na Utamaduni walimtia katika gari na kuondoka naye
kuelekea katika ngome yao huko Boy-Rabe. Mashirika ya kutetea haki za
binadamu ya Umoja wa Mataifa yametahadharisha kuhusiana na kuongezeka
jinai za kivita katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Waziri huyo ametekwa nyara siku moja tu baada ya Rais Bi. Catherine
Samba-Panza wa nchi hiyo kulaani vikali vitendo vya kutekwa nyara watu
nchini humo kunakofanywa na watu waaobeba silaha. Hayo yanajiri katika
hali ambayo, Jamhuri ya Afrika ya Kati imeendelea kushuhudia machafuko
na hivyo kuzorotesha shughuli pamoja na maisha ya kawaida ya wananchi wa
nchi hiyo. Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia kwenye machafuko na
mapigano ya wenyewe kwa wenyewe baada ya kuondolewa madarakani serikali
ya Rais Francois Bozize, mapigano ambayo hadi sasa yamepelekea Waislamu
wengi kuuawa. Kundi la kigaidi la Kikristo la Anti-Balaka limekuwa
likiwalenga kwa makusudi Waislamu wa nchi hiyo katika mashambulio yao.
Maelfu ya Waislamu wa nchi hiyo wamelazimika kuyakimbia makazi yao
wakihofia usalama wa maisha yao.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment