Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Khadija Karamagi.
Wakulima
wa wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro nchini Tanzania wametishia kulivunja
Ghala la wakala wa mazao nchini NFRA kutokana na kutolipwa pesa zao kwa
wakati hali inayowapelekea kushindwa kuandaa mashamba kwa msimu
mwingine.
Wakizungumza
mbele ya katibu tawala wa Wilaya hiyo Severine Garika jana wakulima hao
wamesema kuwa Serikali iliwaahidi kuwa wakala huyo atanunua mazao yao
na kusema mpaka sasa ni zaidi ya miezi minne hawajalipwa pesa zao na
kuwafanya waanze kuishi maisha magumu.
Wakulima hao wamesema serikali imekuwa ikiwazungusha na kuingiza siasa katika suala hilo na kusema kuwa wamefikia hatua ya kushindwa kuwapeleka shule watoto wao kutokana na kutolipwa fedha hizo kutoka kwa wakala huyo.
Kufuatia tamko hilo la wakulima sambamba na maandamano mpaka kwa mkuu wa wilaya hiyo katibu tawala wa wilaya hiyo Bw. Severin Garika ambaye amewataka wakulima hao kuwa na subira kwa kuwa serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za kulipa madeni hayo.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment