
Mtayarishaji wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, Man Walter kutoka
Combination Sound amepandisha bei ya kurekodia katika studio zake
nakufikia shilingi Milioni Moja kwa wimbo ambapo hiyo ni gharama ya
kuanzia.Akiongeana Chanzo kimoja cha habari kwa njia ya simu jana jioni, Man
Walter amesema kuwa sasa ni wakati wa kuangalia upande wa pili wa sanaa
na sio tu kuwaangalia wasanii wanaofanya muziki bila kuwaangalia
wanaoutengeneza muziki huo.
Man Walter amesema kuwa kama watayarishaji wa muziki wakiendelea kutoza
gharama za awali watabaki kuwa maskini huku wasanii wakineemeka kwa kuwa
na kipato kikubwa kitu ambacho si sahihi kwani hawa wote wanatakiwa
wapate maendeleo ya karibu sawa kila mtu kwa nafasi yake.Aidha Man Walter amesema kuwa Milioni Moja kwa wimbo ni bei ya kuanzia
hivyo inaweza kupanda au kushuka inategemeana na aina ya wimbo kwani
atakuwa anatoza kulingana na categories za muziki kwani huwezi
kufananisha wimbo wa Ali Kiba na wimbo wowote wa Hip Hop.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment