Abdu Kiba amesema hayo baada ya Ali Kiba kuonesha uwezo mkubwa katika jukwaa tamasha la Sauti za Busara 2015 lililofanyika February 12-15 visiwani Zanzibar alipotumbuiza kwa Live Band.
Akiongea kwa njia ya simu Abdu Kiba aliyeongozana na Ali Kiba na kutumbuiza pamoja katika tamasha hilo amesema kuwa tamasha Sauti za Busara limekuwa darasa tosha kwao kwani kushiriki katika kwao kumewafanya wajifunze asili ya muziki wa mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uzuri wa kutumia Live Band katika nyimbo zao.
Abdu Kiba amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa wasanii kufanya muziki wa Live ikiwa ni pamoja na kuzirudia nyimbo zao kwa mtindo huo ili kuliteka soko la sanaa duniani kwani ‘Live Music’ ni kila kitu katika soko hilo.
Katika hatua nyingine Abdu Kiba amewashukuru wakazi wa visiwa vya Zanzibar kwa ukarimu na mapokezi mazuri huku shukrani zake nyingine ni kwa waandaaji wa tamasha hilo la Sauti za Busara kwa kuwapa nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo kubwa na la kipekee.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment