February 06, 2015

 
Tareha 14 Feb ni Sikukuu ya Wapendanao. Siku maalumu kwa ajili ya kuoneshana mapenzi ya dhati. Ni siku muhimu sana yenye maana kubwa kwa kila mtu, maana upendo hauchagui.
Maana halisi ya siku yenyewe inaharibiwa na watu wanaotumia fursa ya Valentine’s Day kufanikisha matakwa ya misukumo ya tamaa za miili yao. Kama unabisha nenda gesti ukaulizie chumba leo, kila mahali utakuta kumejaa!
 http://stylespk.com/wp-content/uploads/2013/02/Ferozeh-Valentine%E2%80%99s-Day-Beautiful-Red-Dresses-2013-Collection-for-Girls-2.jpg 
ASILI YAKE NI  NINI?
Asili yake hasa ni Roma. Ni siku ya kumkumbuka mtakatifu Padre Valentino ambaye alifungwa na kuhukumiwa kunyongwa katika  Utawala wa Dola ya Warumi alipokuwa akitetea vijana waoane badala ya kuzini.
Mtakatifu Valentino aliuawa siku na tarehe kama hiyo, ndiyo maana ikatangazwa rasmi kuadhimishwa kwa ajili ya kumkumbuka kama Baba wa Upendo – mtetezi wa wanandoa.
Aliyetangaza rasmi kuadhimisha siku hiyo ni Papa Gelasius.

SIYO NGONO, ANASA!
Baadhi ya watu wameibadilisha maana ya siku hii muhimu kwa wapendanao. Wenyewe wanahisi kuwa ni siku ya kufanya mambo yasiyofaa. Kwao, wapendanao ni ngono. Kuna ambao huanzisha uhusiano siku hiyo kwa lengo la kupata mtu wa kustarehe naye, hili ni kosa.
Kama mtazamo wako ni kutafuta mpenzi mpya na kwenda kustarehe naye utakuwa unakosea sana. Haina maana ya ngono wala anasa na kuharibu fedha kwenye ulevi. Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya kwa lengo la kuifanya siku yako kuwa nzuri.
KUMBUKA NDUGU
Inawezekana unaishi kwenye mji mwingine, kazi zinakubana kila siku na hupati muda wa kuwasiliana mara kwa mara na ndugu zako. Siku hiyo ni nzuri kwako kuwakumbuka na kuwaonesha kwamba unawapenda.
Wapo watu muhimu zaidi katika maisha, wazazi. Mpigie simu mama/baba yako, mwambie unavyompenda na kuthamini malezi aliyokupa hadi kufikia umri ulionao. Kama unaweza watumie hata zawadi kwa ajili ya kuonesha mapenzi yako kwake.
Ondoa fikra mbaya kichwani mwako rafiki yangu. Waza kuhusu mema na kupendana kwa dhati, hapo utakuwa umekwenda sawa na maana ya sikukuu yenyewe.
WAKUMBUKE WAHITAJI
Katika jamii yetu kuna watoto wanaoishi katika mazingira magumu, wazee na wahitaji wengine. Tumia ulichojaliwa kushiriki nao. Siyo lazima iwe fedha, hata chakula na mavazi. Inawezekana una nguo unazodhani hazifai, wape wenzako ambao wanahitaji hapo utakuwa umeonesha namna unavyotambua na kuiadhimisha kwa usahihi.
Ifanye siku hii kuwa ya tofauti zaidi kwa kudumisha uhusiano wako na mpenzi wako na kuzungumzia changamoto mbalimbali za uhusiano wenu kuliko kuwaza starehe na anasa ambazo hupoteza fedha. Niwatakie maandalizi mema ya siku ya Valentine

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE