Wanamgambo wa kitakfiri wa kundi la kigaidi la Boko Haram
wamekishambulia kijiji kimoja huko Niger. Gazeti la Le Figaro
linalochapishwa nchini Ufaransa limeripoti kuwa, watu walioshuhudia
wameeleza kuwa wanamgambo wa Boko Haram wamekishambulia kijiji cha Bosso
nchini Niger kinachopatikana karibu na mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na
Nigeria. Shambulio hilo linatajwa kuwa la kwanza kufanywa na Boko Haram
huko Niger. Watu walioshuhudia shambulio hilo la Boko Haram katika
kijiji cha Bosso nchini Niger wamesema kuwa walisikia sauti za milio ya
silaha nyepesi na nzito. Kundi la kigaidi la Boko Haram lilianza
kutekeleza mashambulizi nchini Nigeria tangu mwaka 2009, na hivi sasa
kundi hilo limekuwa hatari kubwa kwa eneo la kaskazini mashariki mwa
nchi hiyo. Nchi jirani na Nigeria kama Cameroon, Niger na Chad pia
zinakabiliwa na mashambulizi ya kigaidi ya Boko Haram. Umoja wa Afrika
tarehe 30 mwezi uliopita ulipasisha pendekezo la kuasisiwa kikosi cha
wanajeshi 7500 kwa ajili ya kupambana na kundi la kitakfirii la Boko
Haram
February 06, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment