Zanzibar inataka kunufaika na uwezo wa kitaalamu wa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran. Hayo yamesemwa na Rais wa Zanzibar Ali Mohammad Shein wakati
alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif mjini
Zanzibar siku ya Alkhamisi. Katika kikao hicho Shein ameashiria nafasi
muhimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo na hivyo ametaka
msaada wa Iran katika kuboresha sekta ya afya Zanzibar na vile vile
katika ustawi wa kilimo, uvuvi na uimarishwaji elimu za kiufundi
Zanzibar. Kwa upande wake Zarif ameashiria uhusiano wa kale na wa
kihistoria baina ya Iran baina ya mataifa ya Iran na Zanzibar.
Ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa mujibu wa uwezo wake,
iko tayari kuimarisha ushirikiano wake na Zanzibar katika sekta za
utamaduni, uchumi, biashara, kilimo, afya na turathi za utamaduni.
Zarif ameelezea matumaini kuwa katika kikao kijacho cha kiuchumi baina
ya pande mbili kitafanyika kwa mhimili wa kuimarisha uhusiano katika
sekta ya kilimo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekuwa akizitembelea
nchi za Afrika Mashariki kutoka siku ya Jumapili ambapo amefanya ziara
ya kufana katika nchi za Kenya, Uganda, Burundi na Tanzania. Baada ya
kumalizia safari yake hiyo huko Zanzibar nchini Tanzania, Alkhamisi
usiku Zarif alielekea mjini Munich Ujerumani kuhudhuria Mkutano wa
Kimatiafa wa Usalama wa Munich na pia kwa ajili ya mazungumzo ya
nyuklia. Akiwa Munich anatazamiwa kufanya mazungumzo na mawaziri wa
mambo ya nje wa Russia, China, Ufaransa, Uingereza, Marekani na
Ujerumani wanaotazamiwa kuhudhuria kikao hicho.
February 06, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment