Waziri wa maliasili na utalii Mh. Lazaro Nyarandu amefunguka kuhusiana
na taarifa zilizoenea kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa
filamu za Kibongo,Aunty Ezekiel na kwamba ujauzito alionao msanii huyo
ni wa kwake.
Mh.Nyalandu amekanusha habari hizo kupitia kupindi cha leo tena cha
Clouds Fm wakati alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa kipindi hicho
Husna Abdul ambapo pia alikuwa ameambatana na mkewe Faraja Kota.Aidha alisema kuwa habari hizo zilitolewa na gazeti moja la hapa nchini
kuwa waziri huyo atumia mamilioni ya pesa za umma kuponda raha na msanii
huyo,wakati huo alikuwa nchini Marekani kikazi kwa mwaliko wa ubalozi
wa nchini humo ambapo wasanii wawili wa hapa nchini Aunty Ezekiel na
Kassim Mganga nao walikuwa wamealikwa
‘’Kwa mara ya kwanza nilimuona msanii huyo kwenye mwaliko huo na baada
ya hapo nikaondoka zangu sikuonana naye tena hata namba yake sina hapo
ndipo habari zikaenea kuwa nimetembea naye mara mimba aliyonayo ni yangu
kwa kweli nilishangaa sana,’’alisema Nyalandu. ‘’Naamini taarifa hizo
zilizidi kuzungumzwa zaidi na maadui zangu wa kisiasa baada ya mimi
kutangaza nia ya kugombea urais uchaguzi mkuu ujao,’’alisema Nyalandu.
Hata hivyo Faraja akizungumzia kuhusiana na taarifa hizo alisema kuwa hazikumshtua hata kidogo kwa maneno kuhusu mumewe amekuwa akiyasikia sana na ameshayazoea na anampenda sana mumewe.
Hata hivyo Faraja akizungumzia kuhusiana na taarifa hizo alisema kuwa hazikumshtua hata kidogo kwa maneno kuhusu mumewe amekuwa akiyasikia sana na ameshayazoea na anampenda sana mumewe.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment