February 12, 2015

Nahodha wa meli ya Italia afungwa miaka 16 jela 
Mahakama moja nchini Italia imemhukumu kifungo cha miaka 16 jela nahodha wa meli ya kifahari ya Costa Concordia iliyoanguka karibu na ufukwe wa kisiwa cha Giglio huko Italia mwaka 2012. Francesco Schettino alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia, kusababisha meli kuanguka na kuondoka kwenye meli hiyo na kuwaacha abiria wakihangaika kuokoa maisha yao. Watu 32 walifariki dunia kwenye ajali hiyo. Schettino amesema anasikitika kwamba amefanywa mbuzi wa kafara kwenye kesi hiyo ili kulinda maslahi ya kifedha ya mabwenyenye wanaomiliki meli hiyo. Imedaiwa kuwa, matajiri wanaomiliki meli ya Costa Concordia walilipa zaidi ya dola milioni 1 ili kufutiwa mashtaka. Mwendesha mashtaka kwenye kesi hiyo alikuwa ameiomba mahakama impe nahodha Schettino adhabu ya miaka 26 jela lakini mahakimu wakaamua kumfunga miaka 16 gerezani.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE