Ni zaidi ya mara tatu kumekuwa na
mijadala ndani ya Bunge la Tanzania tumesikia ikijadilia kuhusu njia
ambayo inhesaidia kutafuta suluhu ya kudumu kwenye ishu ya tatizo la
wanafunzi shule za Msingi na Sekondari kupata ujauzito.
Leo nimekutana na hii story nikajua
kwamba kumbe tatizo hili sio la Bongo peke yake, Indonesia wao wameenda
mbali zaidi, Jimbo la Java Mbunge mmoja alitoa pendekezo la kuwa na
utaratibu wa kuwapima bikira wanafunzi wa kike wanaomaliza shule za
Sekondari, ambaye akikutwa hana basi safari yake kimasomo itaishia hapo
hatoruhusiwa kuendelea na masomo.
Ni nchi hiyo hiyo mwaka jana ilitoka
ripoti ya utafiti iliyosema kumekuwa na zoezi la kupima bikira askari wa
kike na wanajeshi kitu ambacho kilikosolewa na watu wa haki za
binadamu.
Viongozi wa dini pia walilaumu hilo japo
walisema kuna dalili zote kwamba ishu hiyo imeendelea kufanywa chini
chini kwa siri japo Serikali ilisisitiza kwamba haitoruhusu utaratibu
huu kuwepo katika nchi hiyo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment