
Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel
Macron, anaapishwa hivi sasa, juma moja baada ya kupata ushindi mkubwa
katika marudio ya uchaguzi mkuu wa Urais nchini humo.
Alimshinda pakubwa kiongozi wa chama cha kulia Bi Marine Le Pen.
Bwana
Macron, ambaye aliendesha siasa zake akiunga mkono umoja wa Jumuia ya
mataifa ya Bara Ulaya, ameahidi kufufua uchumi wa Ufaransa na kufanyia
mabadiliko siasa za kale za Ufaransa.

Ili kuafikia mabadiliko zaidi, chama chake kipya cha The Republic on
the Move, kinafaa kushinda viti vingi vya ubunge katika uchaguzi wa
mwezi ujao.
Mwaandishi wa BBC anasema kuwa, iwapo Bwana Macron,
atashindwa katika wadhifa huu wake mpya kama Rais wa Ufaransa, atakuwa
tu sawa na mtangulizi wake wa chama cha Kisosiolosti Francois Hollande,
ambaye aliahidi mabadiliko, lakini anaondoka kama Rais asiye na umaarufu
katika hostoria ya Ufaransa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment