Hatari ya mashambulizi ya mara kwa
mara nchini Pakistani imefanya jamii ya nchini humo kuchukua hatua
ambazo zimeonekana si za kawaida.
Kaskazini magharibi mwa
Pakistani, Polisi wanatoa mafunzo ya namna ya kutumia silaha kwa Walimu
wa shule na Chuo kikuu hatua iliyokuja baada ya Wanamgambo wa Taliban
kuwaua Watu 150 katika Jimbo la Peshawar mwezi Disemba.Wanajifunza namna ya kuweka risasi, kulenga na kufyatua.Silaha wanazotumia ni pamoja na Bastola na Bunduki, pia wanajadili kuhusu mbinu za kujilinda na namna ya kuwalinda Wanafunzi ikiwa Wanamgambo wa Taliban watavamia wakati ambapo watakuwa darasani wakisoma.
Jitihada hizi za mafunzo ya matumizi ya silaha zinatoka katika Serikali ya Jimbo la Khyber-Pakhtunkhwa na Mamlaka ya Polisi, zikiwa ni jitihada za kuimarisha usalama kwenye Shule.
Waziri wa Elimu na Mawasiliano wa Jimbo, Mustaq Ghani amesema Jimbo lina Askari 65,000 lakini hawatoshi kulinda Shule 45,000, taasisi za mafunzo na Vyuo vikuu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment