Raia wawili wa Urusi wanaofanya kazi katika shirika la Utair wametekwa nyara mjini Darfur nchini Sudani, maafisa wameeleza.
Utair
imeingia mkataba wa kusafirisha vifaa vya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa
na Umoja wa Afrika wa kulinda amani Darfur(UNAMID) ambao wamekuwa mjini
Darfur tangu mwaka 2007.Ubalozi wa Urusi mjini Khartoum umethibitisha kutekwa kwa Raia wa Urusi.
Darfur ni mji ambao umekuwa na mgogoro mkubwa kati ya Serikali na Waasi tangu mwaka 2003.
Taarifa ya UTair imesema basi dogo la Unamid lilizuiiwa na Magari sita.Abiria waliokuwamo walishurutishwa kutoka ndani ya Basi kisha wakachukuliwa na kupelekwa kusikojulikana.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment