March 06, 2015

 Matonya na Tunda Man wakiwa Clouds Fm
Lile bifu la zaidi ya miaka nane kati ya wasanii Tunda man na Matonya hatimaye limezikwa rasmi. Leo kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm kinachoongozwa na Husna Abdul (Dahuu) na Geah Habib wamefanya jambo la hilo la Kihistoria kwa kumaliza tofauti hizi za wasanii hawa wakali wa bongo Fleva. Binafsi nichukue fursa hii kutoa pongezi nyingi sana kwa Clouds Media na kipindi cha Leo Tena. Pongezi nyingi kwa Dahuu na Geah Habib kwa busara za hali ya juu kwa kufanya jambo hili jema kwa maslahi ya sanaa yetu. Pongezi kwa Tunda man na Matonya kwa kukubali kufikia maamuzi haya.
Story  kamili ni hii
Tunda Man amesema anachohisi alimkosea Matonya ni kusema kwamba alimtungia nyimbo lakini  hataki tena kuzungumzia ishu hiyo, amesema leo itakuwa mara ya mwisho kuzungumzia jambo hilo na kuomba radhi kwa yote yaliyotokea, hana tatizo lolote na Matonya.
Matonya amesema kuwa Tunda Man ni mdogo wake ambaye wamekutana vizuri na walikuwa wanaishi vizuri lakini alipata wasiwasi baada ya kuona kila siku kuna maneno yanaibuka ambayo hakupendezwa nayo, yeye binafsi anampenda Tunda Man na hata familia yake, kwa nafasi yake kama kaka ameamua kumsamehe.
Tunda amesema hawakuwahi kuonana tangu mwaka 2007.. Matonya akamalizia kwamba kwa sasa wako tayari kwa pamoja kuingia studio kufanya collabo.

Zaidi sikiliza hapa

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE