March 08, 2015

 
Maharagande akipokea fomu za kuwania nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge morogoro mjini kutoka kwa katibu kata ya Sultani Area Amin Kabwanga katikati, wanaoshuhudia tukio hilo kushoto ni M/kiti CUF  Morogoro mjini Abeid Mlapakolona kulia ni M/Kiti CUF Morogoro vijijini Amani Kasnaga 

 Hayawi hayawi sasa yamekuwa, hatimaye mbivu na mbichi za Maharagande zimedhihirika jana TH 7 March 2015. Baada ya taarifa mbalimbali juu ya kuomba ridhaa ya chama chake, hatimaye Mbarala Maharagende amechukua rasmi fomu za kuomba ridhaa hiyo ya kukiwakilisha chama cha wananchi CUF katika nafasi ya ubunge wa jimbo la Morogoro Mjini. 
 Katika tukio hilo lililohudhuliwa na mamia ya wakazi wa Morogoro katika viwanja vya Nyumbani kw akina Maharagande. Mh: Maharagande amechukua rasmi fomu hizo na kuzirejesha jana hiyo hiyo huku akiwataka wakazi wa jimbo la Morogoro Mjini kumuunga mkona katika maamuzi yake hayo.
 
Mh: Maharagande akionesha Form hizo

 
Maharagande akizungumza na wakazi wa JMorogoro mijini baada ya kukabidhiwa Form za kuomba ridhaa ya kugombea ubunge
 Katiaka Hotuba yake Maharagande amesema kazi kubwa ya mbunge ni kuhakikisha anatetea maslahi ya jimbo lake na taifa kwa jumla, kuchangia mijadara mbalimbali bungeni kwa maslahi ya Taifa  na kuhakikisha maendeleo katika jimbo lake yanapatikana na sivinginevyo
  Maharagande ameomba ridhaa hiyo kutoka ndani ya chama chake  na baadaye kutoka katika kambi ya UKAWA imuhidhinishe kuviwakilisha vyama hivyo na kumpata mbunge makini atakayeiwakilisha Morogoro mjini

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE