Bunge la Afrika Kusini litasimamisha shughuli zake wiki ijayo kwa ajili
ya kuendesha mapambano ya kupinga ukatili dhidi ya wageni nchini humo.
Ripoti iliyotolewa jana na bunge hilo imesema kuwa, wiki ijayo bunge
hilo litasimamisha vikao vyake kwa lengo la kuwaruhusu wabunge kwenda
katika maeneo bunge yao na kufikisha ujumbe kwa wananchi ili kukomesha
ubaguzi dhidi ya wageni. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mpango huo
uliopendekezwa na serikali utaweza kusaidia kupunguza wimbi la
mashambulizi dhidi ya wageni waishio nchini Afrika Kusini. Mbali na
mpango huo kutajwa kuwa utasaidia kupunguza wimbi la ubaguzi, unaelezwa
kuwa utasaidia pia kudhamini usalama wa wageni nchini humo. Mashambulizi
dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini yameongezeka katika wiki za hivi
karibuni, kufuatia matamshi ya Mfalme wa kabila la Zulu, Goodwill
Zwelithini, aliyoyatoa mwezi uliopita akiwataka wageni kuondoka nchini
humo. Hadi sasa watu kadhaa wamekwishauawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Tayari Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amelaani vitendo hivyo na
ameshakutana na shakhsia 50 wanaoongoza taasisi za wageni waishio nchini
humo na kujadiliana nao njia za kumaliza tatizo hilo.
April 25, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment