May 25, 2015

 Maria Adili baada ya kupatiwa matibabu

 Askari wa pikipiki maarufu Voda Fasta mkoani Morogoro anahusishwa na tukio la kumgonga  Maria Adili 16 mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika shule ya Sekondary Kingorwila na kukimbia.
Maria Adili akiwa nyumbani kwao
Akuzungumza na ubalozini.blogspot.com baba mzazi wa mwanafunzi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kiswanya ''B'' ndugu Adili omary amesema, ilikuwa Th 21 mei 2015 majira saa kumi jioni, binti yake akitokea shuleni, kufika katika maeneo ya Faya jilani na Hospitali ya sabasaba ndipo alipokutmbwa na ajali hiyo.
 Akiongea kwa uchungu mdugu Adili anasema baada ya binti yake kupatwa na tukio hilo, chakusikitisha zaidi muhusika wa tukio hilo askari wa pikipiki akakimbia kusikojulikana na wamejalibu kufwatilia bila mafanikio.
 "kwakweli hiki ni kitendo cha kinyama sana kwa chombo ambacho tumekipa dhamana ya kutulinda sisi na mali zetu, lakini cha ajabu baada ya huyu bwana kumgonga binti yangu akakimbia na tumefwatilia bila mafanikio mpaka sasa"
 Tulipomuuliza kama mtuhumiwa wa tukio hilo anafahamika Adili amesema ni mtu ambaye anafahamika kila kona na wanazidi kufwatilia kujua nini hatma ya muhusika wa tukio hilo
  Blog hii inalaani vikali kwa tukio hilo la kinyama

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE