
Rais Dk. Jakaya Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Anthony Peter Mavunde
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, kuanzia leo, Jumatatu,
Mei 25, 2015.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uhamisho wa
wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya
mbali mbali nchini.
Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole
Lenga kutoka Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa
wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict Kulikela Kitenga ambaye
alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu, 2015.
Wakuu wengine wa wilaya ambao Rais Kikwete amewahamisha ni Elizabeth
Chalamila Mkwasa kutoka Wilaya ya Dodoma kwenda Wilaya ya Mvomero, Mkoa
wa Morogoro, Dkt. Jasmine Tisike kutoka Wilaya ya Mpwapwa kwenda Wilaya
ya Dodoma, Agnes Elias Hokororo kutoka Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa
Ruvuma kwenda Wilaya ya Tunduru, mkoani humo humo na Fadhili Nkurlu
kutoka Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Mkalama.
Wengine ambao wamehamishwa ni Chande Bakari Nalicho kutoka Wilaya ya
Tunduru kwenda Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka Wilaya ya
Mvomero kwenda Misenyi, Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Wilaya ya
Karagwe, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Biharamulo, mkoani humo humo,
Elias Choro John Tarimo kutoka Wilaya ya Biharamulo kwenda Chunya, Mkoa
wa Mbeya na Deodatus Lukas Kinawiro kutoka Wilaya ya Chunya kwenda
Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera.
Imetolewa na; Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 25 Mei, 2015
0 MAONI YAKO:
Post a Comment