Muigizaji Wema Sepetu ametangaza kuwania Ubunge wa viti maalum Singida
Wasanii wa filamu na muziki wameamua kujitokeza kuwania nafasi za
ubunge katika maeneo mbalimbali nchini katika uchaguzi wa 2015. Mpaka
sasa wasanii waliojitokeza ni wafuatao;
Profesa
Jay, Mikumi- “Nimeamua kugombea jimbo la Mikumi kwa kuwa ni nyumbani.
Wazazi wangu waliishi hapa kwa muda mrefu lakini pia nimekuwa nikiimba
siasa sana na sasa nimeona huu ni muda wa kufanya yale niliyokuwa
nikiimba kuuhusiana na maendeleo ya taifa.”
Dude,
Tabora Mjini- “Nimeanza kufanya maandalizi ya kugombea ubunge nyumbani
kwetu Tabora mjini, niko tayari kuchuana na yeyote na sasa niko kwenye
maandalizi ikiwemo kuwa karibu na wananchi kwani wananikubali, hivyo
nitahakikisha ninapata ushindi.”
JB,
Kinondoni- “Nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia
ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo, ni muda mwafaka sasa wa
kutimiza ndoto yangu ya kuitumikia jamii.”
Soggy
Doggy, SegereaSoggy Doggy ametangaza kugombea ubunge wa jimbo hilo,
jijini Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chadema. Jimbo hilo kwa sasa
linashikiliwa Makongoro Mahanga (CCM)
Steve
Nyerere, Kinondoni- “Ukiona chereko chereko ujue mambo yameiva,
nitagombea ubunge 2015. Nimejipanga na ninaweza kufanya hivyo, nipo
vizuri sana.” Jimbo hilo la Kinondoni liko chini ya Mhe. Idd Azzan (CCM)
Afande
Sele, Morogoro Mjini -“Niliumizwa baada ya kusikia kuwa eti katiba ya
chama cha Chadema inasema kuwa mwanachama anayekwenda mahakamani kudai
haki yake anakuwa amejivua uanachama wake. Kwa chama kama Chadema
sikuamini kama kingekuwa na sheria kandamizi kama hiyo ya kuwazuia
wanachama wake kwenda mahakamani, ndio maana nimeamua nijiunge na chama
kingine ambacho kitakuwa kinamuweka huru mwanachama kudai haki zake.”
Jimbo la Morogoro Mjini kwa sasa lipo chini ya Mohamed Aziz Abood (CCM)
Dokii,
Kilosa Morogoro-“Mimi ni msanii pekee naweza kusema ndiyo nimetumika
sana kwenye jamii kuliko wasanii wote, kwenye kuelimisha jamii najitolea
hata kipindi kile cha madereva wa bodaboda mpaka wakanipa Ubalozi
nilikua natetea haki zao, pia nataka kuonyesha kwamba wanawake
tunaweza.”Jimbo la Kilosa liko chini ya Mustafa Mkulo (CCM) ambaye
aliwahi kuwa Waziri wa Fedha kabla ya kujiuzulu
King
Majuto, Tanga Mjini kwa mujibu wa maneno yake anasema lengo kubwa ni
kutaka kuinua uchumi wa Tanga pamoja na kutetea haki za wananchi pamoja
na rasilimali za Mkoa huo. “Nitarudisha Tanga ya zamani ambayo ilikuwa
ikisifika sehemu mbalimbali kutokana na rasilimali zilizopo ambazo kwa
sasa zimeshindwa kusimamiwa na kuwanufaisha watu wa Tanga.” alisema
Majuto ambaye atakua akichuana na mbunge wa sasa wa Tanga Mjini, Omari
Nundu (CCM)
Shilole,
Igunga, Baada ya Dalali Kafumu anayefuata ni mimi, mimi nadhani napenda
jimbo langu na nawapenda wakazi wangu wa Igunga wananiona tangu nakua
mpaka sasa hivi, kwa hiyo wanafurahi. Sasa wananiambia “sisi hatutaki
kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa na hivyo wananipa changamoto,” alisema
msanii huyo.“Vitu viwili vya kwanza ambavyo nitavifanya nikiingia
kwenye lile bunge nikiwa kama msanii, kwanza nitatetea haki za wasanii,
cha pili Igunga yangu wapo wakazi wa Igunga vijana wapate kazi, yaani
akinamama, wale mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. Kwahiyo
nitawatafutia kazi na nitajenga chuo cha muziki”
Kalapina,
Kinondoni, Kwanza sasa hivi anaitwa Mbunge wa Kinondoni, hivyo
nitagombea uchaguzi ujao. “Kuna mambo mengi ambayo nimepanga kuifanyia
Kinondoni,’’ anasema Kalapina
Mrisho
Mpoto, Ubungo-“Nataka kurudisha heshima, utamaduni na maisha bora kwa
watu wa Ubungo.” Jimbo la Ubungo kwa sasa liko chini ya John Mnyika
(Chadema)
Kingwendu
Mwigizaji Kingwendu, anasema anajiandaa kugombea ubunge mwaka huu
2015.Hata hivyo, Kingwendu hakuweka bayana atagombea jimbo gani wala
kupitia chama gani, isipokuwa zaidi anasema kuwa chama ambacho
kinapendwa na Watanzania wengi ndicho atatumia tiketi yake.Kingwendu
anasema, “Ninajiandaa kugombea ubunge 2015 kupitia chama ninachoona
kinapendwa na Watanzania wengi kwenye jimbo ambalo nitalitaja hapo
baadaye wakati utakapofika, bado ninafanya mazungumzo na washauri wangu
wa karibu kuhusiana na suala hilo, nadhani nitaliweka wazi muda
ukifika.”
Juma
Chikoka, Ilala. Msanii wa sanaa ya maigizo na filamu, Chikoka maarufu
kwa Chopa Mchopanga au Mzee wa Halmashauri ya Kichwa, Mwaka 2010 aliwahi
kuchukua fomu na kujitosa kwenye siasa kwa kugombea ubunge wa Jimbo la
Ilala kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini alishindwa kwenye
kura za maoni za chama hicho na mbunge wa sasa wa jimbo hilo Mussa
Zungu. Mwaka huu wa 2015, amepanga kujitosa tena na safari hii anasema
kuwa kinachomsukuma hadi kuamua kugombea tena ni kutaka kuwawakilisha
vijana wenzake katika ngazi ya juu ya uongozi na kupambana na uhaba wa
ajira kwa vijana.Anasema kuwa yeye ni mzoefu katika siasa, kwani
alishawahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni, mhamasishaji wa vijana,
pia ni mmoja kati ya waanzilishi wa matawi ya CCM nchini India
Chanzo:jamii forum
0 MAONI YAKO:
Post a Comment