Mwalimu Nyerere kama mtu, mwanasiasa, mzazi/ mlezi
na mwanafalsafa Mwafrika, msomi mahiri na kiongozi alikuwa na sura mbili
zisizoshabihiana: Sura ya mafanikio na sura isiyo na mafanikio kama
ilivyo kwa binadamu wengine. Moja ya mambo ambayo Mwalimu hakufanikiwa
ni kujenga wafuasi wa kutosha ndani ya chama alichokiongoza wenye haiba
na hulka yake kwa masuala ya kitaifa. Kwa ajili hii mwandishi mmoja
aitwaye Sarwed amewahi kutamka kuwa Mwalimu alijaa utata, na
ukitendawili!
Mwalimu Nyerere kama mtu, mwanasiasa, mzazi/ mlezi
na mwanafalsafa Mwafrika, msomi mahiri na kiongozi alikuwa na sura
mbili zisizoshabihiana: Sura ya mafanikio na sura isiyo na mafanikio
kama ilivyo kwa binadamu wengine. Moja ya mambo ambayo Mwalimu
hakufanikiwa ni kujenga wafuasi wa kutosha ndani ya chama alichokiongoza
wenye haiba na hulka yake kwa masuala ya kitaifa. Kwa ajili hii
mwandishi mmoja aitwaye Sarwed amewahi kutamka kuwa Mwalimu alijaa
utata, na ukitendawili!
Kwa nini Nyerere hakuacha mrithi mahiri na makini
wa sera zake? Wana taaluma, Kigoda cha Mwalimu, taasisi yake
zinaendeleza mambo yake, lakini siyo chama chake na kwa hakika siyo kwa
kiwango amabacho tungetegemea kukiona katika jamii ya Watanzania ambayo
maeneo ya vijijini bado wana amini yupo, anaishi na bado ni sehemu ya
uongozi wa nchi. Ni kweli Mwalimu hatasahaulika haraka kwa namna yoyote
ile. Uwezo wake wa ushawishi na nadharia ya utu ilifunika upungufu wake
na kwa hiyo ataishi kwa miaka mingine mingi sana. Pia, wanaojaribu
kumfunika ni kama wanapambana na mafuriko kwa mikono – nikitumia maneno
ya mmoja wa wasaka urais kupitia CCM.
Licha ya CCM kuyakimbia mema ya Mwalimu, lugha ya
sasa ya kurejesha uzalendo, utu, uwajibikaji wa viongozi na wa raia
vimeanza kusikika masikioni mwa raia kutoka nyanja mbalimbali na hasa
kwa sasa kupitia chama cha ACT – Wazalendo, ambacho kimeamua pamoja na
mambo mengine kurejesha mambo yote ya msingi na mema ambayo Mwalimu
Nyerere alilitendea taifa hili. Licha ya dhamira hii tofauti kabisa na
ya Chama Cha Mapinduzi, bado Watanzania wachache wanaamini kuwa chama
hiki ni zao la CCM na kwa hiyo hakiwezi kuwa na jipya kama ambavyo
tunataka kuamini kuwa hakuna jipya aliloacha Nyerere.
Nyerere alitetea sana kuondoa umaskini, ujinga na
maradhi. Alijitahidi sana wakati wa uongozi wake kuhakikisha kuwa
wananchi wanaondokana na tabia zinazoondoa asili ya mwanadamu ya
kujiamini, kujiheshimu na kuwa tayari kulitetea taifa kwa kuhakikishiwa
usalama wa elimu, afya, chakula, maji na miundombinu ya kujiendeshea
maisha. Hata hivyo Mwalimu aliiacha nchi ikiwa ndani ya dimbwi la
umaskini mkubwa ambao wachumi wanadai ulizidi umaskini walioacha
wakoloni.
Licha ya umaskini huu wa raia walio wengi na hasa
waishio vijijini, tunaona jinsi ambavyo uongozi umekuwa bidhaa
inayonunulika na kuuzwa katika masoko ya kampeni kwa kuwarubuni maskini
senti chache, vyakula vya siku moja, kufuru za sherehe na hata za
kutangaza tu nia ya kuliongoza taifa, nazo zinatumia mamilioni ya fedha,
huku wengine wakishangilia wakisema mwenzetu huyu kafanikiwa, tazama
anavyoweza kulisha watu wengi kwa siku moja.
Kuna Watanzania wanaoneemeka na umaskini huu kiasi
cha kuishi kwa fedha ya Kitanzania ya zaidi ya milioni kwa siku kwa mlo
– maarufu “fedha za sokoni” kama alivyozitamka waziri wa nyumba, ardhi
na makazi aliyejiuzulu majuzi mbunge Anna Tibaijuka, ambaye naye ni zao
la Mwalimu Nyerere kama mmoja wa wanawake waliopata fursa ya kupata
elimu nzuri bure bila malipo, bila hongo, bila fedha za wazazi wao! Kwa
nini Mwalimu hana mrithi ndani ya CCM?
Kwa kifupi Tunu zote za Mwalimu zimemomonyoka,
hakuna aliye tayari ndani ya CCM kuendeleza kwa dhati mambo aliyoacha
Mwalimu Nyerere. Kwa nini? Kwa nini Mwalimu aache hali hii? Kwa nini CCM
imsaliti Mwalimu wakati akiwa bado hai na baada ya mauti yake? Kwa nini
kila alichosimamia Mwalimu kimeanguka na ni kama inabidi nchi kuanza
upya badala ya kuendeleza?
Tatizo liko wapi na ni nini hasa? Je, ni Mwalimu
au ni sisi Watanzania kutokuwa na Mwalimu kuweka misingi ya utawala wa
nchi yetu; kushindwa kuweka mfumo wa utawala ambao yeyote akiingia
madarakani angeendeleza badala ya kuanza upya? Ni mahali gani Mwalimu
alikosea njia na kuingia msitu mnene usiotoa dira ya utawala wa kutukuka
kama ambavyo wengi tungedhani kutokana na umahiri wake?
Kama Baba wa Taifa na nikimlinganisha na mababa
wengine wa nchi mbalimbali duniani, Nyerere aliweka kitu kinachotakiwa
katika nchi. Alifanikiwa kuiwekea Tanzania taswira ya utaifa
iliyoeleweka na kuheshimika duniani. Misingi ya utu, uzalendo, umoja wa
kitaifa, kupinga ubaguzi, kuheshimu utu wa mtu na hata kuwajali
wanawake, na kuwapa fursa za upendeleo katika elimu na uongozi ili
kujenga usawa wa fursa kwa jinsi zote mbili. Ninadiriki kufikiri kuwa
Mwalimu alikosa mlezi ndani na nje ya chama chake na ama alifurahia hali
hii kwa kumfanya kinara wa kila jambo, ama hakujitokeza Mtanzania wa
aina ambayo Mwalimu angemheshimu kumpa nafasi ya kumlea kiroho na
kiakili.
ili afanikiwe katika mambo ambayo hakuwa na uwezo
nayo. Pamoja na hayo yote bado kitendawili kinabaki na swali kuwa kwa
nini Mwalimu hana mfuasi wa kweli ndani ya chama chake?
Kwa nini mara tu alipotoka madarakani CCM ikaanza
kuyumba na kuonesha kabisa kuwa haikuwa na utashi na utawala wa muasisi
wake? Sera za maendeleo za baada ya Mwalimu, si tu zilisukumwa na mfumo
wa dunia wa uchumi, lakini pia zilisukumwa na hali ya kupotea, kukosa
dira, kukiuka maadili ya uongozi, hali ya viongozi kutaka kuwarubuni
wananchi nyakati za uchaguzi kwa kutumia rushwa kupata uongozi, wizi wa
wazi wa mali za umma na matumizi mabaya ya nafasi za uongozi, makundi
yanayohasimiana ndani na nje ya vyama.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment